Home BUSINESS RC CHALAMILA AFANYA ZIARA KIWANDA CHA NAMELA TEXTILE LIMITED

RC CHALAMILA AFANYA ZIARA KIWANDA CHA NAMELA TEXTILE LIMITED

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Novemba 12, 2024 amefanya ziara ya kushitukiza kiwanda cha nguo na mavazi cha Namela Textile Limited kilichopo Gongolamboto Jijini Dar es Salaam.

RC Chalamila amefanya ziara hiyo kwa lengo la kujionea kiwango cha uzalishaji, Ubora wa bidhaa pamoja na malalamiko au changamoto zizokikabili kiwanda hicho.

Aidha RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kutokana na juhudi kubwa anazozifanya kutika kuboresha mazingira ya uwekezaji hapa nchini, kwa kuwa uwekezaji licha ya kukuza pato la taifa, hutoa ajira lakini pia ni chanzo cha fedha za kigeni.

Sanjari na hilo RC Chalamila ameahidi kufanya ziara rasmi katika kiwanda hicho akiwa na timu ya wataalamu mbalimbali kwa lengo la kufikia suluhu ya changamoto zilizotolewa ikiwemo kuingia kwa bidhaa za magendo na kukosekana kwa malighafi pamba.

Ifahamike kuwa kiwanda hicho kime ajiri wafanyakazi zaidi ya 1500 na uwekezaji wake ni Dola milioni 70 sawa na TZS zaidi ya Bilioni 150.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here