Home LOCAL NI VYEMA TAMISEMI IKAANGALIA UWEZEKANO WA KUWARUDISHA WAGOMBEA WENYE MAKOSA MADOGO MADOGO-...

NI VYEMA TAMISEMI IKAANGALIA UWEZEKANO WA KUWARUDISHA WAGOMBEA WENYE MAKOSA MADOGO MADOGO- DKT NCHINI

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiomba Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kuwaelekeza wasimamizi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kupuuza makosa madogo madogo yaliyotokea, ili kuruhusu wagombea wengi kushiriki uchaguzi huo.

Akizungumza na wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo vya hahari nchini, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametoa mfano wa makosa hayo yanayostahili kupuuzwa ni pamoja na wagombea kukosea herufi.

Kupitia mkutano huo uliofanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, leo Novemba 12, 2024, Balozi Nchimbi amesema ni vyema TAMISEMI ikaangalia uwezekano wa kuwarudisha wagombea wote walioenguliwa kutokana na makosa hayo madogo madogo ili kuhamasisha ukuaji wa demokrasia kwenye uchaguzi huo.

Aidha, kuhusu sehemu kubwa ya malalamiko mengi ya kuenguliwa kuonekana ni ya wagombea wa vyama vya upinzani, Balozi Nchimbi amewatoa shaka Watanzania kuwa, si kweli kwamba wagombea walioenguliwa ni wale wa vyama vya upinzani pekee, bali pia hata wagombea wa CCM wapo waliowekewa mapingamizi ya kugombea.

“Waziri wa TAMISEMI tunajua anafuata sheria, lakini ni muhimu kutambua demokrasia yetu hii bado ni changa hivyo tunahitaji muda wa kuendelea kujiífunza…tunaziomba mamlaka hasa TAMISEMI katika nyakati za mwisho za rufaa kuyapuuza makosa madogo madogo ili watu wengi wapate nafasi ya kugombea”, alisema Dkt. Nchimbi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here