Home INTERNATIONAL NCAA YATANGAZA UTALII NCHI ZA UJERUMANI, JAMHURI YA CZECH, AUSTRIA NA POLAND.

NCAA YATANGAZA UTALII NCHI ZA UJERUMANI, JAMHURI YA CZECH, AUSTRIA NA POLAND.

Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) inashiriki maonesho ya utalii yajulikanayo kama ‘My Tanzania road show’.
yanayoshirikisha baadhi ya Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii (TAWA,TANAPA,NCAA) na Kampuni binafsi zinazojihusisha na utalii chini ya uratibu wa kampuni ya Kili Fair iliyopo mkoani Arusha.

Maonesho ya Tanzania my Road show yamefunguliwa katika mji wa Frankfurt nchini Ujerumani na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Iddi Mwamweta tarehe 11 Novemba, 2024 na yatahitimishwa katika mji wa Warsa, Poland tarehe 15 Novemba,2024 ambapo NCAA inawakilishwa na Afisa Utalii Jemima Billiah

Maonesho haya yanalenga kukutana na makampuni mbalimbali ya utalii katika nchi hizo na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania pamoja na maeneo ya uwekezaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here