Home INTERNATIONAL DKT. ASHATU KIJAJI ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAZINGIRA AFRIKA (AMCEN)

DKT. ASHATU KIJAJI ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAZINGIRA AFRIKA (AMCEN)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameshiriki Mkutano wa Mashauriano wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika (AMCEN) leo Novemba 17, 2024.

Mkutano huo ni wa pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa (COP29) unaoendelea jijini Baku, Azerbaijan.

Katila mkutano huo mawaziri wamejadili masuala ya mazingira pamoja na upatikanaji wa fedha za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Pia, Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira ni sehemu ya mkakati wa kuweka msimamo wa pamoja wa nchi za Afrika kwenye majadiliano yanayoendelea kwenye COP29. 

Katika mkutano huo, Waziri Mhe. Dkt. Kijaji ameambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Lujemeja na wataalamu.

http://DKT. ASHATU KIJAJI ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAZINGIRA AFRIKA (AMCEN)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here