Home LOCAL CHAGUA CCM KWA MAENDELEO HADI MLANGONI KWAKO

CHAGUA CCM KWA MAENDELEO HADI MLANGONI KWAKO

Na: Mwandishi Wetu, Tanga.

Wananchi wamesisitizwa kuwachagua wagombea watokanao na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuharakisha maendeleo katika mitaa yao.

Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Tanga Mjini (CCM), Ummy Mwalimu Novemba 25, 2024 wakati akiwanadi wagombea wa CCM kutoka mitaa ya Kange (Kata ya Maweni), Pongwe Kusini (Kata ya Pongwe) na Mapojoni (Kata ya Kirare).

Sambamba na hilo, Ummy Mwalimu amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuwachagua wagombea na wajumbe wao huku akisisitiza wasidharau uchaguzi huu kwani mipango ya maendeleo inaanzia ngazi ya mitaa yao.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga, Ustadhi Rajabu Abdurahman akiwa katika mkutano wa hadhara mtaa wa Kange, kata ya Maweni amesema kwa kazi nzuri zilizofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika mkoa wa Tanga, anaamini CCM itashinda vijiji, vitongoji na mitaa yote kwa asilimia 100 kwa mkoa wa Tanga.

http://CHAGUA CCM KWA MAENDELEO HADI MLANGONI KWAKO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here