Home INTERNATIONAL WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MAADHIMISHO YA SIKU YA FIMBO NYEUPE.

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MAADHIMISHO YA SIKU YA FIMBO NYEUPE.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 25, 2024 amewasili mkoani Kilimanjaro ambapo anamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe na Miaka 60 ya Chama cha Wasioona Tanzania (TLB).

Siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe huadhimishwa kila Oktoba 25 kwa lengo la Kuelimisha jamii kuhusu haki na uwezo wa watu wenye ulemavu wa kuona, Kutambua umuhimu wa fimbo nyeupe katika kusaidia watu wenye ulemavu wa kuona kusafiri kwa usalama na uhuru na hatimaye kufikia malengo yao.

Aidha, Siku hiyo pia ina lengo la kuhamasisha ujumuishaji wa watu wenye ulemavu wa kuona katika jamii na kuhakikisha wanapata fursa sawa katika elimu, ajira, na huduma zote nyingine.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Upatikanaji wa Teknolojia Saidizi na Fikivu ni Mkombozi kwa Uchumi Endelevu kwa Mtanzania asiyeona.”

Previous articleTANZANIA YAPIGIWA MFANO, KUKABILI MAAFA, MATUMIZI SAFI YA NISHATI YA KUPIKIA YATAJWA
Next articleBALOZI NCHIMBI AWAFARIJI MZEE MAKAMBA NA FAMILIA YA MWAMBI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here