Home LOCAL WAFUGAJI WAMETAKIWA KUACHA KUFUGA KWA MAZOEA

WAFUGAJI WAMETAKIWA KUACHA KUFUGA KWA MAZOEA

NA FARIDA MANGUBE

Wafugaji wametakiwa kuachana na ufugaji wa mazoea badala yake watumie ushauri wa wataalamu wa afya ya mifugo ili kuongeza uzalishaji utakao leta tija kwa wafugaji sambamba na kudhibiti magonjwa.

Ushauri huo umetolewa na Rasi wa Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Esron Karimuribo wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo na vyeti kwa wanafunzi waliohitimu na kufanya vizuri kwenye masomo yao.

Profesa Karimuribo amesema hakuna tija kwa mifugo kama wafugaji wanaendelea kufuga kienyeji na kutumia tiba zisizo za uhakika huku akiwataka wanafunzi hao kwenda kuwasaidia wafugaji kwa kutumia mafunzo waliyoyapa chuoni hapo.

Hata hivyo amewataka wanafunzi hao kutumia vyema taaluma waliyoipata SUA kuwahudumia wafugaji na mifugo sambamba na kutengeneza fursa kwa kujiajiri na kuajiri wengine ili kuondokana na dhana potofu ya kutafuta ajira.

“Ndugu zangu tunatambua kuwa vijana mlio wengi mnasoma mara tu mnapo hitimu mafunzo mnakimbilia kuanza kutafuta ajira badala ya kutengeneza wenyewe ambazo hata hivyo zinaweza kuwasaidia vijana wengine” Amesema Profesa Karimuribo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Masomo ya Shahada za Awali SUA Dkt. Hamza Tindwa amewataka wafugaji kutumia wataalamu kutoka SUA kwani ndiyo Chuo pekee kinacho toa wataalamu wenye weledi.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi waliopata tuzo ya kufanya vizuri katika masomo Zainabu Yasini ameishukuru SUA kwa kuwapa taaluma bora itakayowawezesha kuendesha maisha yao na kuwasaidia wafugaji kufuga kwa tija huku akiwataka vijana kuwekeza zaidi kwenye taaluma walizosomea.

Previous articleMPASUKO MKUBWA ALIOUACHA LISSU IKUNGI: MBINU ZA UPINZANI KUGAWA WATU ZAFICHUKA
Next articleSERIKALI YAWEKA MKAZO KUKUZA TASNIA YA UFUGAJI WA KUKU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here