Home LOCAL VYUO VIKUU VYASHAURIWA KUWEKEZA KWA VIJANA

VYUO VIKUU VYASHAURIWA KUWEKEZA KWA VIJANA

Vyuo vikuu hapa nchini vimeshauliwa kuwekeza kwa vijana kwa kuwapatia mitaji wakiwa bado wanafunzi ili waweze kuendeleza mawazo ambayo wanayo ili kujiari na kupunguza wimbi la kukosekana kwa ajira pindi wamalizapo masomo pia kuweza kuwaajili vijana wenzao.

Hayo yamebainishwa na umoja wa wanafunzi ambao walisha wahi kusoma Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ikiwa na lengo la kukumbushana mambo mbalimbali ambapo wamevishauri vyuo vikuu hapa nchini kuona namna yakuwasaidia wahitimu wao mitaji ili waweze kujiajiri na kuacha kusubiri kuajiriwa na kuyafanyia kazi mawazo yao waliyotoka nayo Chuo pia kuwapatia ajira vijana wengine.

Aidha, wameuomba uongozi wa SUA kuwekeza zaidi kwa kutoa elimu ya vitendo kwa wanafunzi ili waweze kupata ujuzi wakutosha.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof, Raphael Chibunda akaeleza lengo la kukutana na umoja wa wanafunzi ambao walishawahi kusoma kusoma Chuo hicho.

Prof, Chibunda amesema kuwa, Chuo kimeandaa mazingira wezeshi ambayo yatamwezesha mwanafunzi kufanya vizuri ambapo pia ameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa fedha kiasi cha shilingi takribani bil 70 kwa kuwekeza katika miundombinu.

Naye Mratibu wa Majalisi wa SUA, Prof. Jonathan Mbwambo akaeleza kwenda kuufanyia kazi ushauri huo uliotolewa na umoja wa wanafunzi hao na kwamba umoja huo utakuwa chachu ya kuimalisha na kuboresha maendeleo ya Chuo hicho.

Previous articleWIZARA YA MADINI KUREJESHA MINADA YA NDANI NA KIMATAIFA MADINI YA VITO
Next articleKUKOSA MISIMAMO KUNAWAGHARIMU CHADEMA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here