Home SPORTS SERIKALI YA UONGOZI CHINI YA  RAIS SAMIA INA KIU KUONA UBANGUAJI KOROSHO...

SERIKALI YA UONGOZI CHINI YA  RAIS SAMIA INA KIU KUONA UBANGUAJI KOROSHO UNAONGEZEKA -MHE MWINJUMA 

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Hamis Mwinjuma, amewahimiza Watanzania kuendelea na utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza na kuimarisha afya zao.

Rai hiyo ameitoa Oktoba 26, 2024, Mkoani Mtwara, wakati akiongoza mbio za “Korosho Marathon” na kukagua mabanda mbalimbali ya wadau wa mbio hizo.

Mhe. Mwinjuma amewaeleza washiriki wa mbio hizo kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ina kiu kubwa ya kuona ubanguaji wa korosho nchini unaongezeka, ili kufikia asilimia 60 ya korosho zinazozalishwa nchini na uzalishaji wa korosho ghafi ufike tani 700,000 ifikapo mwaka 2025/26, kama ilivyoainishwa katika ilani ya CCM 2020-2025.

Mbio hizo zilizoandaliwa na Bodi ya Korosho Tanzania zina lengo la kuchangisha fedha za hisani zitakazoelekezwa katika kuboresha usindikaji wa korosho kupitia vikundi vya wanawake na vijana. Aidha, fedha hizo zitatumika kuboresha sehemu za masoko wanayoyatumia kuuza bidhaa zao na kukuza fursa za ajira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here