Home INTERNATIONAL MTANZANIA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA DUNIA

MTANZANIA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA DUNIA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), akimpongeza Dkt. Zarau Wendeline Kibwe, kwa kuchaguliwa na Benki ya Dunia kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika, inayojumuisha nchi 22 ikiwemo Tanzania, nafasi ambayo Tanzania imewahi kuihudumu miaka 54 iliyopita kupitia kwa Mtanzania mwingine, Bw. Christopher Kahangi, kati ya mwaka 1968 – 1970. Tukio hilo limetangazwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Benki ya Dunia wa Kanda Namba Moja ya Afrika, uliofanyika wakati wa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF na Benki ya Dunia inayofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (katikati), akiwa na Viongozi wengine, Waziri wa Fedha wa DRC- Congo, Mhe. Nicolas Kazadi (wa pili kulia), Waziri wa Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum (wa pili kushoto, Balozi wa Tanzania-Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza (kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha- Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji anayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika, aliyemaliza muda wake, Bw. Floribert Ngaruko (kulia) akiwa katika picha na Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Kundi hilo la Kanda namba Moja ya Afrika ya Benki ya Dunia kutoka Tanzania, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe, baada ya kutangazwa rasmi katika Mkutano wa Mwaka wa Kanda hiyo kushika wadhifa huo, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF, Washington D.C-Marekani)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here