Home LOCAL DC SAME AONGOZA WANANCHI SAME  ZOEZI LA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUPIGA KURA

DC SAME AONGOZA WANANCHI SAME  ZOEZI LA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUPIGA KURA

Na Ashrack Miraji – Fullshangwe Media

Mkuu wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni, amesema kuwa zoezi la uandikishaji wananchi kwenye Daftari la Mkazi linaendelea kwa mafanikio, huku wananchi wengi wakiwa wamehamasika na tayari wameshajiandikisha kwenye vituo mbalimbali.

DC Kasilda alitoa kauli hiyo Oktoba 11, 2024, baada ya kujiandikisha mwenyewe katika Daftari la Mkazi kwenye Kituo cha Stesheni, kilichopo katika Kata ya Stesheni. Kituo hiki ni mojawapo ya vituo 503 vya uandikishaji vilivyopo Wilayani Same.

Aidha, DC Kasilda aliwasisitiza wakazi wa Same kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vilivyoko katika maeneo yao ili kujiandikisha, hatua ambayo itawapa uhalali wa kushiriki katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here