Home SPORTS CHAN 2025 NA AFCON 2027 MAANDALIZI YAPAMBA MOTO

CHAN 2025 NA AFCON 2027 MAANDALIZI YAPAMBA MOTO

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya ziara ya kukagua miundombinu ya michezo katika uwanja wa Shule kuu ya Sheria na uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Jijini Dar es Salaam ambavyo vitatumika kwa mazoezi wakati wa mashindano ya CHAN 2025 na AFCON 2027.

Katika ziara hiyo ambayo Mhe. Ndumbaro akiwa ameambatana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema kuwa, hadi sasa hatua iliyofikiwa inakidhi vigezo kuelekea katika mashindano hayo.

Ikumbukwe kwamba kwa mara ya kwanza Tanzania, Kenya na Uganda watakuwa wenyeji wa mashindano hayo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here