Home LOCAL CHAMA CHA MAPINDUZI CHAMUONYA MWENYEKITI WA  ACT WAZALENDO

CHAMA CHA MAPINDUZI CHAMUONYA MWENYEKITI WA  ACT WAZALENDO

Na Leluu Majjid, JamhuriMedia, Zanzibar

Chama cha Mapinduzi kimemkanya Makamo Mwenyekiti wa ACT_Wazalendo Ismail Jussa Ladhu na kumtaka aachane na fikra za kizamani na kutaka kukirithisha kizazi kipya siasa za enzi za ASP na Hizbu.

Ametakiwa kuacha mpango huo kwani zama za siasa hizo zimepita na kubaki historia isiohitajika na kizazi cha sasa .

Matamshi hayo yametamkwa na katibu wa kamati maalum ya Nec itikadi na Uenezi ,Khamis Mbetto Khamis aliyemtaja jussa kama mtu ambaye hakuwepo enzi hizo hivyo hana sababu ya kukilisha maneno ya chuki kizazi kipya.

Mbetto alisema Jussa anafikiri ACT kitaungwa mkono na wananchi kwa kutaka kwake muungano uliopo uvunjike, zanzibar ipate mamlaka kamili au kwa kuzusha huku akidai serikalini (SMZ) kuna ubadhirifu mkubwa.

Aliisema kama Jussa ana ushihidi wa kutosha dhidi ya madai yake, amemtaka afungue mashitaka mahakamani ili awaowatuhumu waweze kushitakiwa kwa madai yake iwapi kuna ufisadi na kuporwa fedha za umma .

Acha siasa za ubaguzi na uchonganishi. Sisi sote hatukuwepo enzi za ASP na Hizbu. Kuzugumzia hadithi zilizochakaa ni kuonyesha kuchakaa kwa mawazo yako . Kuwa muungwana .Acha kuchafua majina ya wenzako “alisema Mbetto.

Aidha Mbetto alisema kabla ya mwaka 1963 serikali ya Zanzibar haikuwa na uwakilishi wa wananchi wenyeji wa Unguja na pemba hivyo kushabikia dola ya Zanzibar enzi za ukoloni ni kutamani ukoloni urudi .

Kusifu dola ya Zanzibar iliokuwa na mawaziri wazungu na waarab chini ya wafalme wahamiaji ni aibu.Serikali halali ya Wazanzibari wenyeji ni bile ya Januri 12 1964 chini ya mzee Abeid Amani Karume “alisema mbetto.

Katibu huyo mwenezi alimtaka Jussa asijipe uwakala wa kutetea mambo asioyajua kwani ufalme wa Zanzibar haukuwa wa kina Pandu ,Makame na Jecha bali ulihamia na kuishi anzibar kimabavu.

Alisema ASP ilifanya mapinduzi mwaka 1964 baada ya kuona uhuru uliotolewa mwaka 1963 hati za uhuru akikabidhiwa mfalme jamsheed bin Abdullah badala ya Mohamed shamte Hamad huku katiba ya mwaka 1962 akimtaja mfalme kuwa ndiye mkuu wa nchi.

“Unadai Zanzibar ilikuwa na sarafu yake wakati noti zina picha ya malkia wa uingereza. Benki kuu haikuwepo Zanzibar. Hati za kusafiria zilikuwa na nembo ya mwingereza.Polisi wa kiingereza na Zanzibar ikilindwa na Jeshi la Uingereza” alisisitiza .

Mbetto alimtaka Jussa na wenzake kufanya siasa za kiungwana ambazo hazitakuwa na hekahela wala misukosuko kwani tabia yake ya kutoa madai ya uzushi yanawadhalilisha baadhi ya wanasiasa wenzake .

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here