Home LOCAL DOTO MAGARI AWATAKA CHADEMA KUACHA SIASA ZA UPOTOSHAJI, AMPONGEZA RAIS SAMIA KUIMARISHA...

DOTO MAGARI AWATAKA CHADEMA KUACHA SIASA ZA UPOTOSHAJI, AMPONGEZA RAIS SAMIA KUIMARISHA AMANI

Na Mwandishi wetu

Mfanyabiashara maarufu wa magari nchini, Dotto Keto maarufu kama ‘Dotto Magari’, amesema. Kuwa ni muhimu kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuachana na siasa za upotoshaji na kumpongeza Rais Samia kwa juhudi kubwa anazozifanya kwa maslahi ya Taifa katika kudumisha amani nchini.

Magari amesema “Nyinyi majirani zetu mlikuwa hamna ofisi kwa takribani miaka 30, leo Mama kajitahidi katoa fungu kawahamishieni ofisi na kupelekwa Mikocheni mnataka nini majirani?”

Aidha Magari amewataka CHADEMA kumuunga mkono Rais Samia kwa kutengeneza mazingira bora ya kuvutia wawekezaji na ya kufanyia biashara nchini.

“Mnasema nchi haina amani, ni amani gani mnayoitaka? Wawekezaji wamerudi, watu wanafanya wanachotaka,hata nyie mnaongea mnachojisikia,  hiyo siyo amani? . Mama anafanya kazi kubwa, ameshughulikia umeme, maji, treni ya umeme, barabara kujengwa kwa viwango na viwanda, mpeni Rais Samia maua yake kwani anafanya mengi kwenye hii nchi”

“Mkikaa kwenye vikao vyenu kuweni wakweli kwamba mama Samia ndiyo kila kitu, apewe mitano yake na akija tena apewe mitano mingine jumla 10, huyu mama ndiyo aliyeweza kuiongoza hii nchi” amesisitiza

Previous articleMHE.GWAJIMA AZINDUA MATAWI YA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUHAMASISHA KUPAMBANA NA VITENDO VYA UKATILI.
Next articleBASHE APONGEZA KAZI NZURI ZA ASA – NZEGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here