Home LOCAL DKT.PHILIP AMEWASIHI WANANCHI KUTUMIA VYEMA MIUNDOMBINU YA BARABARA ILIYOJENGWA NA SERIKALI

DKT.PHILIP AMEWASIHI WANANCHI KUTUMIA VYEMA MIUNDOMBINU YA BARABARA ILIYOJENGWA NA SERIKALI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewasihi wananchi kutumia vema miundombinu ya barabara inayojengwa na serikali ili kuepusha ajali zinazopelekea madhara makubwa.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akizungumza na waumini mara baada ya kushiriki Ibada ya Kawaida ya Asubuhi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Amani Kijiji cha Kasumo mkoani Kigoma. Amesema ujenzi wa Barabara kiwango cha lami katika maeneo mbalimbali ikiwemo kijijini hapo utapelekea kuongezeka kwa vyombo vya moto vya usafiri hivyo ni muhimu kujifunza na kuwafundisha watoto namna bora ya kutumia barabara hizo.
Aidha Makamu wa Rais amesema ujenzi wa miundombinu ni gharama hivyo wananchi wanapaswa kutunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Halikadhalika Makamu wa Rais amewahimiza wananchi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Amesema zoezi hilo ni muhimu kwa kuwa linatoa fursa ya kupata viongozi wanaoishi na wananchi katika maeneo yao. Amewaasa kuchagua viongozi bora watakaojitolea kushughulikia changamoto za wananchi kuliko maslahi binafsi.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
26 Septemba 2024
Kigoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here