Dar-es-Salaam Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imefanya kikao Cha mashauriano ya wadau kuhusu mkataba wa Sheria ya Kimataifa ya (WIPO) ya Ulinzi wa maumbo na michoro ya miliki ubunifu.
Akizungumza na wanahabari, Leo, Septemba, 5, 2024, Bw.Godfrey Nyaisa ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) amesema Tanzania ni Moja ya Nchi wanachama wa shirika la miliki ubunifu Duniani (WiPO) na shirika la miliki ubunifu la Kanda ya Afrika (ARIPO) kupitia mashirika haya Nchi ya Tanzania, imesaini na kuridhia mikataba na itifaki mbalimbali zinazohusu usimamizi na uratibu wa miliki ubunifu kikanda na masuala mengine.
“Mikataba na hitifaki hizi zimewekwa mifumo Katika kuhakikisha usimamizi na uratibu thabiti wa miliki ubunifu Kimataifa ili kuendana na mabadiliko yanayoendelea duniani hasa Katika nyanja ya teknolojia na ubunifu, Nchi wanachama wa WIPO zimeendelea kuandaa mikakati na njia za kuhakikisha miliki ubunifu inatumika kama chachu ya maendeleo Duniani hii imefanyika kwa kufanya majadiliano kwa kukabiliana kuanzisha Mikataba Katika maeneo muhimu ya umiliki ubunifu.
“Kwa Sasa Kuna ushindani mkubwa wa kibiashara Nchini na nje ya mipaka ya Nchi hasa Katika kuongeza ubora wa bishaa au huduma na muonekano unaovutia wa bidhaa hivyo tunatakiwa kuhakikisha bidhaa zetu ikiwemo vifungashio na mikebe zinakuwa na ubunifu wa kipekee tunatakiwa kuhakikisha bidhaa au huduma ina muonekano unaovutia,” amesema Bw.Nyaisa.
Pia ameongeza kuwa watakwenda kufanya mafunzo kwa wanafunzi ili kuwajengea uwezo vijana wadogo ili mtoto awe na uelewa kuhusu ubunifu.
Nae Mr. Mustafa Haji msajilii msaidizi kutoka ( BPRA) ambaye amumuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji BPRA Bw.Khamis Juma amesema kuwa sekta nzima inayohusina na miliki ubunifu Tanzania bara na Zanzibar inafanya kazi zake Katika kuhakikisha inashirikiana na mamlaka husika ili kuweza kupiga hatua gurudumu la maendeleo na uchumi kwa ujumla.
“Tumekuwa tukifanya kazi kwa pamoja Katika kutoa elimu,kushirikiana Katika Mikataba mbalimbali ya Kimataifa na Kitaifa kuhakikisha kwamba Tanzania inachukua kuona miliki ubunifu inafanikiwa kwa kiasi kikubwa,” amesema Mr.Haji.