Home LOCAL BIASHARA YA KUUZA MAJI HAITAKUWEPO TENA WILAYA YA UBUNGO-MHE.LUKUVI

BIASHARA YA KUUZA MAJI HAITAKUWEPO TENA WILAYA YA UBUNGO-MHE.LUKUVI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi amesema biashara ya kuuza maji katika Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, haitakuwepo tena baada ya Mradi wa Maji ya Mshikamano kukamilika katika wilaya hiyo kwa asilimia 100.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara leo baada ya kufanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Ubungo, Lukuvi amesema kero kubwa ya wananchi wa Mbezi ilikuwa ni maji na kwamba watu walikuwa wakilazimika kununua maji na kuifanya biashara ya maji kuwa nzuri.

Amesema Mradi wa Maji ya Mshikamano umegharimu zaidi ya bilioni 4/- na kwamba utahudumia zaidi ya watu laki mbili katika wilaya hiyo.

Lukuvi amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo huo wa maji pamoja na mradi wa ukamilishaji wa jengo la ghorofa ya pili katika Kituo cha Afya Kimara.

Amesema huduma katika sekta ya afya Wilaya ya Ubungo inapatikana kwa asilimia 100. Amesema, kimsingi serikali imeleta fedha nyingi za maendeleo kwenye wilaya hiyo na hivyo maendeleo katika wilaya hiyo ni makubwa kutokana na serikali kutekeleza vyema sera za Chama Cha Mapinduzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here