Home BUSINESS WIZARA YATOA NENO ASALI YA TANZANIA SASA KURUHUSIWA KUUZWA CHINA

WIZARA YATOA NENO ASALI YA TANZANIA SASA KURUHUSIWA KUUZWA CHINA

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesaini makubaliano ya kuruhusiwa kuuza asali yake nchini China huku ikisisitiza pia uwepo wa mikakati yenye lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao yanayotokana na nyuki.

Akizungumza leo Agosti 15,2024 jijini Dar es Salaam katika hafla ya Tanzania na China wakisaini mkataba wa asali ya Tanzania kuruhusiwa kuuzwa katika nchi hiyo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dustan Kitandula amesema kutokana na uwepo na mwitikio wa sekta binafsi katika kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya ufugaji nyuki, mwaka 2018 ,Tanzania ilianza mawasiliano na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa lengo la kufungua soko la asali la China.
Uganda.

Aidha, wastani wa tani 793.5 za nta inayozalishwa nchini huuzwa katika masoko ya Japan, Amerika, Poland na Ujerumani. Mauzo hayo ya Asali na Nta nje ya nchi huipatia Tanzania wastani wa Dola za Kimarekani milioni 12.9 sawa na shilingi bilioni 30.58 kwa mwaka.

Kitandula amesema kutambua fursa kubwa ya biashara ya asali na mazao mengine ya nyuki, Serikali imeweka mikakati madhubuti ili kuongeza kiwango cha uzalishaji na ubora wa asali pamoja na kuongeza mauzo ya asali na mazao mengine ya nyuki nje ya nchi.

Amesema moja ya mikakati hiyo ni kuweka mazingira rafiki kwa soko la Asali katika nchi za Umoja wa Ulaya na Uingereza, kwa kuweka na kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Udhibiti wa Mabaki ya Kemikali katika Asali.

Mpango huu unalenga kuhakikisha asali inayozalishwa nchini inakidhi viwango vya ubora vinavyohitajika na masoko ya kitaifa, kikanda na kimataifa.Pia Serikali imeweka mfumo wa ufuatiliaji wa ubora wa asali unaojulikana.Mfumo huu unatumika kutunza na kutoa taarifa za wazalishaji na wafanyabiashara wa mazao ya nyuki,”amesema.

Kwa upande wake Waziri na Katibu wa Kamati ya CPC ya Utawala Mkuu wa Forodha ya Watu, Jamhuri ya China Yu Jianhua amesema mkakati wa China ni kuwa karibu na Tanzania kutokana na urafiki wa kimkakati wa miaka mingi baina ya nchi mbili hizo.

Hiki kilichotokea leo ni mwendelezo wa historia ya miaka mingi ya uhusiano baina ya China na Tanzania, tumeingia makubaliano ya itifaki kununua asali kutoka Tanzania, lakini ninaamini kuna mengi zaidi tutayafanyaa,” amesema.

Previous articleDKT JAFO: KILA MKOA KUANZISHA VIWANDA
Next articleWAZIRI JAFO ATAKA KILA MKOA KUANZISHA VIWANDA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here