Home LOCAL WAZIRI MAVUNDE:ZIARA YALETA FARAJA KWA WACHIMBAJI WADOGO LEMISHUKO,SIMANJIRO MANYARA

WAZIRI MAVUNDE:ZIARA YALETA FARAJA KWA WACHIMBAJI WADOGO LEMISHUKO,SIMANJIRO MANYARA

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amefanya ziara kukagua shughuli za uchimbaji madini na kusikiliza changamoto za wachimbaji wadogo katika eneo la Lemishuku,Wilayani Simanjiro eneo ambalo ni maarufu kwa uchimbaji wa madini vito ya Green Garnet

Waziri Mavunde amepata nafasi ya kukagua uwekezaji uliofanywa katika uchimbaji wa madini katika Kijiji cha Lemishuku na kuahidi kwamba Serikali itafanikisha urushwaji wa ndege nyuki “drone” katika eneo hilo kwa ajili ya utafiti wa kina ili kuwaongoza vizuri wachimbaji wadogo kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha na kuongeza kuwa mwishoni mwa mwezi Desemba 2024 jengo la kituo cha ununuzi wa Madini litakuwa limekamilika ili kufanikisha urahisi wa Biashara ya madini.

Aidha,Waziri Mavunde alieleza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan itatatuwa Changamoto zote za Maji,Umeme,Barabara na Zahanati ili kuchochea shughuli za ukuaji wa sekta ya madini ambapo katika ujenzi zahanati aliongoza harambee ambayo jumla ya matofali 4500,sarufi mifuko 183 na fedha Tsh 23m zimepatikana.

Akitoa salamu zake Mbunge wa Simanjiro, Mh. Christopher Ole Sendeka, amemshukuru Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kazi kubwa ya kuboresha huduma za kijamii katika eneo hilo la uchimbaji na kumshukuru Waziri Mavunde kwa kuwa Waziri wa kwanza kufika katika eneo hilo kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo (FEMATA) John Bina na Mwenyekiti wa Mabroka Tanzania (CHAMATA) Ndg. Jeremiah Kituyo wameipongeza serikali kupitia wizara ya madini kwa mipango ya uendelezaji wa sekta ya madini na kusisitiza kwa wachimbaji wadogo kuzingatia sheria za nchi na pia kwa wafanyabiashara wa madini kuhakikisha wanakata Leseni ya biashara ya madini ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro,Mh. Fakhi Lulandala amewahakikishia wachimbaji wadogo wa eneo la Lemishuku kwamba Serikali ya ngazi ya Wilaya kupitia Taasisi mbalimbali zilizopo hapo zitahakikisha zinasimamia kwa ukaribu utekelezaji wa changamoto za wachimbaji ili kuweka mazingira mazuri ya uchimbaji katika eneo la Lemishuku.

Previous articleMH.RAIS ALIPOWASILI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA SHEIKH AMRI ABEID
Next articleDkt. BITEKO APONGEZA JITIHADA ZA CRDB BANK MARATHON KUSAIDIA WATOTO, WAKINAMAMA NA VIJANA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here