Home ENTERTAINMENTS STARTIMES KUENDELEA KUUNGA MKONO LIGI YA CHAMPIONSHIP

STARTIMES KUENDELEA KUUNGA MKONO LIGI YA CHAMPIONSHIP

KAMPUNI ya Startimes imesema itaendelea kuunga mkono Ligi ya Championship ili kuwapa nafasi vijana kuonesha vipaji na kujiuza kimataifa.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa masoko na maudhui kutoka Startimes David Malisa kwenye uzinduzi wa kampeni mpya ya zote ndani.

Malisa amesema wanatarajia kuonesha Ligi kubwa za Ulaya zikiwemo La Liga ya Hispania, Ujerumani Bundesliga, Saudi Arabia, Carabao Cup na Copa Del Rey.

“Ligi zote kubwa zitakuwa Startimes, tunaanza nyumbani na Championship kisha kimataifa na hiyo yote tunataka mashabiki zetu waendelee kubaki na sisi kwa kulipia vifurushi kwa bei ndogo na kuona namna vijana mbalimbali wanavyofanya vizuri,”amesema.

Meneja wa vipindi na Maudhui kutoka Tv3 Emmanuel Sikawa amesema michuano hiyo yote itaruka kupitia Tv3 na kuhimiza mashabiki wa soka na wadau mbalimbali kutobaki nyuma bali ni wakati sahihi kuona vipaji vya soka vya ndani na kimatifa.

Amesema wamekuwa wakifanya vizuri kuonesha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kwa asilimia 75 lakini pia, wamekuwa wakionesha michuano tofauti ya Afrika na lengo ni kuhakikisha watu wanapata burudani na kujifunza namna wengine wanafanya.

“Tunajua kuwa mashabiki wengi wanapenda mpira na awamu hii tutakuwa tunachambua, tutawafuata mashabiki mahali walipo kuona wananufaika vipi na michezo hii,”alimalizia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here