Home SPORTS SIMBA SC YAFANYA MAKUBWA TAMASHA LA SIMBA DAY

SIMBA SC YAFANYA MAKUBWA TAMASHA LA SIMBA DAY

Wachezaji wa Kikosi cha Simba Sc wakishangilia goli wakiwa katika mchezo wa kirafiki wa kuhitimisha Tamasha la 16 la Simba DAY uliopigwa katika dimba la Benjamini Mkapa Agosti 3, 2024, Dar es Salaam, katika mchezo huo wamefanikiwa kuibuka na  ushindi wa mbao 2 -0 dhidi ya APR ya Rwanda 

DAR ES SALAAM

Wekundu wa Msimbazi Simba Sc wamefanikia kuibuka na ushindi wa mbao 2 -0 dhidi ya APR ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa kuhitimisha tamasha la 16 la Simba DAY uliopigwa katika dimba la Benjamini Mkapa Agosti 3, 2024, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba Sc yamefungwa na kiungo wao mpya Debora Fernandez Mavambo mwenye uraia pacha wa Kongo Brazaville pamoja na Angola katika dakika ya 46.

Huku bao la pili likifungwa na Mshambuliaji Edwin Charles Balua dakika 66, huu ni mchezo wan ne mfululizo Simba Sc inashinda chini ya kocha mpya Fadluraghman ‘Fadlu’ Davids.

Katika tamasha hilo mashabiki wa Simba Sc walijiokeza kwa idadi kubwa na kuujaza uwanja wa Benjamini Mkapa, ambapo tukio hilo liliambatana na utambulisho wa kikosi kipya cha timu hiyo ambacho kitashiriki michuano ya msimu wa 2024/2025.

Previous articleMKULIMA KWETU NI MDAU MKUBWA  – PURA
Next articleTARI YAWAKARIBISHA WADAU MAONESHO YA NANENANE -2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here