Home LOCAL MHE.DKT NDUGULILE MGOMBEA NAFASI YA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI...

MHE.DKT NDUGULILE MGOMBEA NAFASI YA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI KANDA YA AFRIKA

Mgombea nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile akijinadi mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 74 wa WHO leo Agosti 27, 2024 unaofanyika katika Jiji la Brazzaville nchini Congo.

Dkt. Ndugulile amesema vipaumbele vyake katika kazi hiyo endapo atachaguliwa kuwa ni kuhakikisha Watu wanapata haki ya kupata huduma bora za afya; Kuboresha utayari wa nchi za Afrika katika kukabiliana na majanga ya magonjwa ya mlipuko, Kuimarisha uwajibikaji ndani ya WHO kanda ya Afrika pamoja kuimarisha mawasiliano baina ya nchi wanachama katika masuala ya Afya.

Zoezi la uchaguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika unafanyika leo kupitia Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afya Afrika chini ya Shirika la Afya Duniani.

Previous articleREA YATOA SHUKRANI KWA  WARATIBU WA MIRADI YA NISHATI VIJIJINI
Next articleMHE.DKT  PHILIP MPANGO AWAOMBA NMB KUENEZA ELIMU YA BIMA KWA WATUMIA VYOMBO VYA MOTO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here