Home BUSINESS MCHECHU; KIKAO KAZI CHA WAKUU WA TAASISI KUANGAZIA UTEKELEZAJI FALSAFA YA R4...

MCHECHU; KIKAO KAZI CHA WAKUU WA TAASISI KUANGAZIA UTEKELEZAJI FALSAFA YA R4 ZA RAIS SAMIA

Na; Mwandishi wetu, ARUSHA

Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu amesema kuwa kikao kazi cha Wakuu wa taasisi na wenyeviti wa Mashirika ya Umma kinachotarajiwa kufunguliwa rasmi Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Agosti 28,2024 Jjijini Arusha, kinakwenda kuangazia Mageuzi makubwa aliyoyafanya kufuatia Falsafa yake ya R4 za Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Ujenzi mpya.

Mchechu ameyasema yao kwente mkutano na waandishi wa habari kilichofanyika leo Agosti 27,2024 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC, Jijini humo.

Amesema kuwa katika Kikao cha mwaka jana Mhe. Rais aliwapa maelekezo kadhaa ya kimsingi yakiwemo mabadiliko katika taasisi za umma na utendaji wake ambayo yanaendelea kufanyika, nakwamba mpaka sasa kuna mabadiliko makubwa katika taasisi hizo.

Aidha Mhe. Rais aliagiza kufanyike maboresho ya taasisi hizo ili ziweze kujiendesha ambapo sasa tayari kuna 48 kati yao yana uhuru wa kujieendeaha yenyewe. Sambamba na hilo aliagiza kwenda kusimamia Mashirika ambayo serikali ina hisa ndogo pamoja na taasisi zote ziweze kuchangia katika mfuko wa serikali kwa kutoa gawio kila mwaka.

“Taasisi zilizochangia mwaka huu wa fedha ulioisha ziliongezeka kutoka 109 hadi 145 ambapo ni ongezeko la taasisi 36. Ninaamini kwamba katika mwaka huu wa fedha kutakuwa na taasisi nyingi zinazoenda kuchangia kwenye mfuko wa Taifa amesema Mchechu.

Ameongeza kuwa kikao cha mwaka huu kimejikita katika kuzisukuma taasisi za umma kuanza kufikiria kuwekeza nje ya mipaka ya Tanzania.

Amesema ili taasisi hizo ziweze kuyafikia malengo hayo zinatakiwa kuweka mikakati ya juu, nakwamba lazima iwe imejihimarisha vizuri ndani ya nchi yake.

“Hivyo tunapowataka waanze kwenda nje maana yake wawe na malengo yaliyo juu zaidi ili kwamba hata ukifeli usiwe chini kabisa ya lengo, bali uwe kwenye nafasi nzuri.

“Ukiangalia makampuni makubwa mfano ya china yaliyowekeza hapa Tanzania, ni yale ambayo kule kwao yanamilikiwa na Serikali, kwa hiyo sisi hatuna sababu ya makampuni yetu kushindwa kuwekeza huko“ amesema.

Pia mchechu ameeleza kuwa katika kikao hicho watakwenda kuangalia mabadiliko ya sheria ikiwa ni agizo la Mhe. Rais ambapo katika kikao kilichopita aliwataka kufanyike mabadiliko ya sheria, na kubainisha kuwa mabadiliko hayo yanakwenda kuzaa vitu kadhaa vya kimsingi vitakavyosaidia kufikia mabadiliko makubwa ya kiuchumi.

“Katika Sheria hii kuna mabadiliko ambayo tumeyafanya ambayo, ni pamoja na upimaji wa ufanisi wa kazi, ambapo sasa hivi kila taasisi ya Umma tunaiangalia katika vigezo vitano.

“Vigezo hivyo, ni pamoja na unavyochangia faida na kutumia mali ulizonazo kuongeza faida, au kupunguza utegemezi wa Serikali, pili ni namna unavyowajibika katika kutekeleza zile shughuli zako za kisekta. Vigezo vingine tunakuangalia kwenye utawala bora, na namna unavyoishi, na kuwahudumia wafanyakazi wako unaowaongoza na kuwasimamia, na mwisho ni jinsi unavyo wahudumia wateja amesema

Amesema kuwa katika mabadiliko ya sheria hiyo wanaangazia suala zima la mtaji ambalo litakuwa ndani ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, au ndani ya Mamlaka ya uwekezaji, nakwamba mfuko huo utakuwa unatunza mitaji kwaajili ya kuzisaidia taasisi ili kama inataka kutekeleza miradi yake, Serikali iwe na uwezo wa kuwasaidia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here