Home LOCAL MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO LA ALMASHAURI WILAYA YA CHEMBA

MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO LA ALMASHAURI WILAYA YA CHEMBA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Wilaya ya Chemba kwaajili ya kuzindua Jengo la Ofisi ya Halmshauri ya Wilaya hiyo akiwa ziarani mkoani Dodoma tarehe 21 Agosti 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Halmshauri ya Wilaya Chemba wakati akiwa ziarani mkoani Dodoma tarehe 21 Agosti 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa watanzania kuwekeza katika elimu kwa watoto ikiwemo elimu ya dini kwa lengo la kukabiliana na mmomonyoko wa maadili unaolikabili Taifa hivi sasa.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Chemba akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi mkoani Dodoma. Amesema ili Taifa liweze kupiga hatua za haraka linahitaji wananchi waliopata elimu.

Amesema kila mzazi na mlezi ni wajibu kusimamia na kuhakikisha watoto wanajengwa katika maadili mema kwa kupata mafundisho mazuri ya dini.

Halikadhalika Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kutunza mazingira ikiwemo kukomesha ukataji miti ovyo, kuacha kuchoma moto wakati wa kuandaa mashamba ya kilimo pamoja na uharibifu wa vyanzo vya maji. Amesema athari ni kubwa zinazotokana na uharibifu wa mazingira ikiwemo kuanza kupata magonjwa, vifo vya Wanyama na binadamu, ongezeko la joto na ukosefu wa maji.

Amewahimiza viongozi kusimamia zoezi la upandaji miti hususani wakati mvua zitakapoanza na kusimamia miti hiyo kuhakikisha inafikia lengo.

Makamu wa Rais pia amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati safi ya kupikia. Ameongeza kwamba serikali imedhamiria kuanzisha mfuko maalum ili kuweza kutoa ruzuku na kuwawezesha wananchi wa kawaida kutumia majiko ya gesi.

Amehimiza Taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kwa siku kuanza kutumia nishati safi ya kupikia kwa kuachana na ukataji miti kwaajili ya kuni na mkaa wa kupikia.

Amewasihi wananchi wa Wilaya ya Chemba kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuzingatia kutunza amani iliyopo nchini.

Awali Makamu wa Rais akiwa wilayani Chemba amezindua Mradi wa Jengo la Ofisi ya Halmshauri ya Wilaya Chemba ambao umegharimu shilingi Bilioni 4.6. amewataka watumishi kulitunza jengo hilo ili liweze kutumika kwa muda mrefu.

Mradi wa Jengo hilo unatarajiwa kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi wa Wilaya hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here