Home LOCAL KAMATI YA TAMISEMI YARIDHISWA NA MIRADI YA MAPATO YA NDANI – KINONDONI

KAMATI YA TAMISEMI YARIDHISWA NA MIRADI YA MAPATO YA NDANI – KINONDONI

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Justine Nyamoga amesema Kamati imeridhiwa na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa kupitia Mapato ya Ndani ya Halmashauri ya Kinondoni.

Mhe. Nyamoga ameyasema hayo katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Ukaguzi wa Miradi inayojengwa kwa Fedha zitokanazo na mapato ambayo ni Shule ya Msingi Richard Mghana, Stendi ya daladala na Jengo la Kitega Uchumi Mwenhe, Uwanja wa Mpira wa Kiszsz, Barabara ya Jamirex na shule ya Sekondari Songoro Mnyonge katika Manspaa ya Kinondoni.

Amesema Kamati imeridhishwa na Utekelezaji wa Miradi hiyo kwani thamani ya fedha inaonekana katika miradi yote iliyotekelezwa na fedha za mapato ya ndani zimewesha ujenzi wa miradi mikubwa na yenye Tija kwa wananchi wa Kinondoni na mkoa kwa ujumla.

Halmashauri nyingi hazitekelezi miradi mikubwa kwa kutumia mapato ya ndani lakini hapa Kinondoni ni tofauti mmeteleza miradi ya mabilioni kutoka kwenye mapato yenu na thamani ya fedha inaonekana kwenye miradi hii hongereni sana amesema.

Aidha Mhe Nyamoha ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa maeneo ya ujenzi majengo mengi sasa yanatakiwa kujengwa kwa mfumo wa ghorofa hivyo wabunifu wa majengo kwenye Halmashauri zetu wanapaswa pia kuzingatia miundombinu hiyo.

Pia Mhe. Nyamoga ameitaka Ofisi ya Rais TAMISEMI kuendelea kusimamia ujenzi wa miradi hii ya maendeleo inayozingatia miundombinu rafiki kwaajili ya walemavu ili nao waweze kunufaika na miradi hiyo kwa urahisi wakati wanapotaka huduma katika maeneo hayo.

Akiwawakilisha wananchi Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu. Josephat Gwajima amesema kumekuwa na Ushirikia mkubwa sana baina ya wananchi na viongozi wa Halmashauri ya Kinondoni jambo ambalo limekuwa kama Chachu katika maendeleo ya Halmashauri hiyo.

Akitoa neno la shukrani Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainab Katimba ameishukuru kamati kwa kuamua kufanya ziara katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliotolewa na kamati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here