Home LOCAL GLOBAL EDUCATION LINK YATOA VISA 100 KWA WANAOENDA KUSOMA NJE YA NCHI

GLOBAL EDUCATION LINK YATOA VISA 100 KWA WANAOENDA KUSOMA NJE YA NCHI

Na,Mwandishi Wetu

WAKALA wa Elimu Nje ya Nchi, Global Education Link (GEL), imetoa Visa 100 kwa kundi la kwanza la wanafunzi wanaotarajia kuanza kwenda kwenye vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi kuanza masomo hayo kuanzia wiki ijayo.

Hiyo inakuja ikiwa zimepita wiki mbili tu tangu matokeo ya kidato cha sita kutoka ambapo mamia ya wanafunzi wa Tanzania wenye kuhitaji kusoma nje ya nchi kupitia GEL wameshaanza kufanya maandalizi ya kuondoka kuanzia wiki ijayo.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Global Education Link Abdulmalik Mollel, wakati akigawa Visa 100 kwa wanafunzi wanaotarajiwa kuondoka wiki ijayo na amezungumza na wazazi na wanafunzi wanaotarajiwa kwenda nchini humo.

Mollel alisema lengo la mkutano huo ni kukabidhi Visa, kujadili na wazazi na wanafunzi kuhusu mambo mambo mengi ya kuzingatia katika maandalizi ya safari, kuwakutanisha wazazi na wanafunzi na wawakilishi wa vyuo vikuu ambavyo wanafunzi hao wanatarajia kwenda kusoma pamoja na wanafunzi kujaza nyaraka mbalimbali.

Leo tumekutana na wanafunzi hawa kuwapa viza zao ambazo zimekamilika kuwapa bima za afya kuwaeleza tarehe za kusafiri ndege watakazotumia kusafiria, kujua sehemu watakazokaa, watasafiri na nani na watapokelewa na nani,” alisema Mollel

“Wataanza kuondoa kwenda kwenye vyuo vikuu mbalimbali duniani kuanzia wiki ijayo na baada ya hapo kila wiki kundi la wanafunzi kuanzia 50 mpaka 70 watakuwa wanaondoka kwenda mataifa mbalimbali,” alisema Mollel.

Mollel awataka wanafunzi kuzingatia walichofuata nje ya nchi na kuachana na starehe na badala yake wazingatie masomo na kuhakikisha wanahitimu wakiwa na alama nzuri ili kuwapa moyo wazazi ambao wamajinyima kwaajili ya kuwalipia ada.

Alisema baadhi ya wanafunzi wamekuwa na kawaida ya kufanya mambo ambayo yanasababisha washindwe kumalizia masomo yao hali ambayo inawakatisha tamaa wazazi wao.

“Msiende kunywa pombe wala kwenda klabu za usiku kwasababu kule mnakwenda kufuata elimu. Malizeni masomo mpate kilichowapeleka starehe hata Tanzania zipo,” alisema Mollel

Aiman Mohamed kutoka Mwanza ambaye anatarajia kwenda masomoni nchini India wiki ijayo, alisema anashukuru uratibu uliofanywa na Global Education Link na kumwezesha kupata chuo cha Sharda cha nchini India.

“Kwa dhati kabisa niwapongeza waratibu wa safari yetu Mollel na wenzake kwa namna walivyokuwa karibu nasisi wakati wote wa kuratibu safari na hatimaye mambo yamekuwa mazuri na wiki ijayo tunasafiri kwenda masomoni kutimiza ndoto zetu,” alisema

Rita Nichalaus naye kutoka Mwanza ambaye anatarajia kujiunga na chuo kikuu cha Sharda kilichoko New Delhi India alisema amefurahi kupata elimu ya mambo ambayo wanatakiwa kufanya na ambayo hawatakiwi kuyafanya wanapokuwa masomoni.”

Mwongozo tuliopewa ni muhimu sana kwasababu mwanafunzi anapofika ugenini asipofahamu tabia na tamaduni za wenyeji anaweza kujikuta yuko matatizoni lakini tumeelezwa namna ya kuishi tukiwa huko ni jambo jema na la msingi sana kwetu,” alisema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here