Home LOCAL TEF YATOA RAI KWA WATANZANIA KUTOSAMBAZA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI

TEF YATOA RAI KWA WATANZANIA KUTOSAMBAZA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) linafuatilia kwa karibu tabia iliyoibuka hivi sasa ya baadhi ya watu kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu kuuawa au kutekwa kwa watoto katika maeneo mbalimbali nchini.

“Yamekuwapo matukio kadhaa ya taarifa za aina hii katika maeneo ya Jiji la Dares Salaam, huko Kigamboni, Mbagala na Kipawa, ambayo yameleta taharuki kubwa hadi wazazi wakafuata watoto shule, lakini baadaye ikathibitika kuwa siyo kweli”
“Tabia hii ya kupokea na kusambaza tarifa ambazo hazina uhakika au ukweli, husababisha taharuki, usumbufu, na mshtuko kwa wazazi, walezi, watoto, na wananchi kwa ujumla”
TEF inawaomba Watanzania kutoa taarifa ambazo wana uhakika nazo ili kuepuka kusababisha taharuki na hofu kubwa.
“Tunaomba wananchi wasisambaze taarifa ambazo hawana uhakika nazo au kufahamu undani wa ukweli wake, kwani ni kosa la jinai kisheria na siyo maadili ya uandishi wa habari kuisumbua jamii”
“Tunatoa wito kwa wazazi na walezi kutimiza wajibu wao wa kuwatunza na kuwalinda watoto wao” 
“Polisi ni wakati tunawasihi kuchunguza matukio yanayotajwa, tunawataka waongeze ulinzi katika maeneo mbalimbali nchini ili kuendelea kuaminika kwa wananchi na wajione wako salama”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here