Home LOCAL “JAMII ISHIRIKIANE NA DOLA DHIDI YA UTEKAJI WA WATOTO” PROF KITILA

“JAMII ISHIRIKIANE NA DOLA DHIDI YA UTEKAJI WA WATOTO” PROF KITILA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo na amewataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki na Wazazi kuwalinda watoto wao wakati wote.

Ametoa tamko hilo akiwa katika ziara yake Kata ya Makurumla iliyopo kwenye Jimbo la Ubungo baada ya kuzuka wimbi la upotevu wa watoto katika maeneo mbalimbali nchini huku wakidaiwa kuwa wanatekwa na watu wasiojulikana katika siku za karibuni

“Leo asubuhi (jana Jumatatu) tumeamka na taharuki katika Kata ya Makurumla na Mburahati kuwa watoto wametekwa mashuleni, tumetoa taarifa kwa vyombo vya dola jambo hili linafanyiwa kazi, uchunguzi ufanyike na jambo hili likomeshwe” Prof. Kitila

Prof. Kitila amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha Kwa vyombo vya dola ili jambo hilo lidhibitiwe kama lipo wahusika wachukuliwe hatua na kama ni taharuki tu nayo ijulikane na hali ya kawaida iendelee.

“Nchi nzima hii kuna jambo la kuteka watoto wadogo linasikika, Kuna kaupepo ka kishetani kanaendelea hapa, tuchukue tahadhari, inavyoonekana siyo kama zamani wakati tukikua Sisi, mtoto alikuwa wa kijiji na mtaa lakini sasa hivi mambo yamebadilika, kuna watu wachache katika jamii yetu kwa kuwa na tamaa aidha ya kupata Mali mali kwa njia za mkato wanateka watoto, kila mtu amlinde mtoto wake” Prof. Kitila

Waziri huyo amewataka wananchi kila mmoja kwa imani yake aliombee Taifa ili hili jambo lisiendelee na hali katika jamii iwe ya utulivu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here