Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amechangia Shilingi Milioni 10 kwaajili ya kumalizia ujenzi wa Ofisi ya Chama Wilaya Mtwara vijijini wakati alipokuwa katika ziara wilayani humo.
Akiwa ziarani Dkt. Nchimbi amesalimia na kizungumza na wananchi wa jimbo la Mtwara Vijijini kata ya Mpapura ambalo liko upinzani.
Amesema kuwa licha ya jimbo hilo kuwa upinzani lakini utekelezaji wa Ilani ya CCM ni wa wakiwango cha juu na wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
“Pamoja na kwamba Jimbo hili liko upinzani lakini utekelezaji wa Ilani hapa ni wakiwango cha juu kwani tumeweka Kaimu Mbunge Mhe Chikota anaefanya shughuli hapa hakika kazi Imefanyika, nafikiri mmeona sasa kazi kwenu.
“Wakati ukifika inabidi mbadilike kwani mnapata maendeleo lakini hamna wa kumhoji, pamoja na yote CCM inawafanyia mambo makubwa tumeyasikia hapa wenyewe sasa wakati ukifika pigeni chini wasiobadilika kichagueni Chama cha Mapinduzi” amesema Dkt. Nchimbi.
Aidha katika ziara yake aliyoambatana na wajumbe wa Sekretarieti wa CCM amewataka wananchi kuendelea kutunza na kuilinda amani ya nchi, nakwamba asitokee mtu kutaka kuharibu amani iliyopo.
29 Julai,2024. Siku ya pili
#VitendoVinasauti
#TunaendeleanaMama
#Kaziiendelee