Home Uncategorized BASHE: MSIUZE MASHAMBA, TUNZENI ARDHI

BASHE: MSIUZE MASHAMBA, TUNZENI ARDHI

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amemuelekeza Afisa Kilimo wa Kata ya Mwamkulu kuhakikisha anasimamia na kuhamasisha wakulima kujisajili kwa wingi katika mfumo wa ruzuku ya mbolea.

Waziri Bashe ameanza ziara yake ya kikazi tarehe 19 Julai 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi na kuweka jiwe la msingi la Ujenzi katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mwamkulu yenye ukubwa wa hekta 3000 ambazo zitanufaisha wakulima takribani 20,000.

“Serikali imewekeza fedha nyingi, ni lazima kuwe na uwajibikaji wa kuhakikisha wakulima wananufaika. Kwa mfano, idadi ya wakulima waliojisajili kupata mbolea za ruzuku, kiasi cha uzalishaji na aina ya mazao ili ijulikane katika kufikisha huduma vijijini,” amesisitiza Waziri Bashe. 

Pia Waziri Bashe amewaomba Wakulima wa Mpanda na Mkoa mzima wa Katavi kutouza ardhi. “Mradi huu ni wa kwenu. Msiuze mashamba. Tunzeni ardhi yenu isaidie vizazi vijavyo. Serikali imegharamia karibia Shiilingi Milioni 10 kwa kila hekta inatumika ili kuwasaidia shughuli zenu za uzalishaji na pia maeneo ya mifugo kupata maji.”

Aidha, ameelekeza Idara ya Maendeleo ya Mazao kuhakikisha kuwa ngazi za Mikoa na Halmashauri za Wilaya kufuatilia utendaji wa Maafisa Ugani kwa kutumia mfumo Maalum ambao umewekwa kwenye vishikwambi vinavyosambazwa na Wizara ya Kilimo kwa Maafisa Ugani. Pia amemuelekeza Mkurugenzi wa Idara ya Zana za Kilimo katika Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa baada ya uzinduzi wa usambazaji wa trekta na “power tiller” mwezi Agosti 2024 zisambazwe kwa Wakuu wa Wilaya ikiwemo Mpanda ili kusaidia shughuli za kilimo kwa wakulima.

Waziri Bashe amelakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Mhe. Jamila Yusuf kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi. Akitoa salamu za Mkoa, Mhe. Jamila ametoa shukrani kwako na Wizara kwa ujumla kwa kuleta miradi ya ujenzi wa skimu za umwagiliaji kwa wakulima wetu ambayo ni skimu ya Mwamkulu kwa gharama ya Shilingi Bilioni 31.6 na skimu ya Usese kwa ajili ya ukarabati kwa gharama ya Shilingi Bilioni 1.2.”

Previous articleWAZIRI BASHE ATANGAZA NEEMA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KATAVI
Next articleBASHE AKABIDHI BONDE LA LUICHE KWA MKANDARASI UJENZI SKIMU YA UMWAGILIAJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here