Home BUSINESS UBIA WA TWIGA MINERALS NA BARRICK WAZIDI KULETA MANUFAA, YATOA GAWIO LA...

UBIA WA TWIGA MINERALS NA BARRICK WAZIDI KULETA MANUFAA, YATOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 53.5 KWA SERIKALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan akipokea hundi ya gawio kutoka kwa Meneja wa Barrick nchini,Melkiory Ngido (Kulia)
Baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali katika hafla hiyo
Viongozi wa taasisi mbalimbali na wageni waalikwa katika hafla hiyo.
 
Katika kudhihirisha kuwa ubia kati ya kampuni ya Barrick Corporation na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals unaendelea kunufaisha pande zote mbili ,Twiga imetoa gawio la bilioni 53,482,072,393 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutunukiwa tuzo ya nafasi ya pili kwa kutoa gawio kubwa mwaka huu.
 
Hundi ya gawio hilo (Dummy cheque) ilikabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido, katika hafla ya Serikali kupokea gawio kwenye makampuni ambayo ina hisa nayo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam
 
Mwaka uliopita Twiga ilishika nafasi ya kwanza kutoa gawio kwa Serikali ya kiasi cha shilingi bilioni 84 katika mwaka wa fedha 2022/23.
 
Migodi iliyopo chini ya kampuni ya Barrick na Twiga Minerals nchini ni North Mara , Bulyanhulu na Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa.
 
Kampuni ya Twiga mbali na kutoa gawio nono kwa Serikali imekuwa ikichangia pato la serikali kupitia malipo ya tozo mbalimbali katika halmashauri zinazotozwa katika maeneo yenye shughuli za migodi yake sambamba na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa kupitia kodi, ushuru, magawio, mishahara na malipo kwa wazabuni wa ndani.
Previous articleBRELA YATOA GAWIO LA BILIONI 18.9 KWA SERIKALI
Next articleTFFT YAENDESHA MASHINDANO YA UBUNIFU KWA SHULE 11 ZA ARUSHA NA KILIMANJARO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here