Home BUSINESS TANZANIA INA UMEME WA KUTOSHA KUFANYA SHUGHULI ZA KIUCHUMI- DKT. BITEKO

TANZANIA INA UMEME WA KUTOSHA KUFANYA SHUGHULI ZA KIUCHUMI- DKT. BITEKO

*Asisitiza hakuna mgawo wa umeme*

 *Amshukuru Rais Samia kuiimarisha Sekta ya Nishati*

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, kwa sasa nchi ina umeme wa kutosha kuwawezesha Watanzania kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Juni 9, 2024 wakati alipoungana na Waumini wa Kanisa la AIC Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita kwenye ibada ya jumapili.

“Nashukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia ameweka mipango madhubuti kwenye sekta yetu ya nishati ambayo sasa imepelekea tuwe na umeme wa kutosha na hatuna mgawo wa umeme.” Amesema Dkt. Biteko

Ameongeza kuwa, miezi michache iliyopita, tatizo la mgawo wa umeme lilikuwa likimkosesha amani, lakini kwa juhudi za viongozi Wakuu wa Serikali, Wizara na TANESCO limefikia tamati.

Kutokana na uwepo wa umeme mwingi wa kutosha, Dkt. Biteko amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo na kwamba Serikali inaendelea kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Previous articleWAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA ITALIA NCHINI TANZANIA ANAYEMALIZA MUDA WAKE
Next articleELIMU YA FEDHA KUIBUA MABADILIKO YA KIFEDHA KIGOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here