Home BUSINESS MATI SUPER BRANDS LIMITED YADHAMINI MASHINDANO YA WEST KILI TOUR CHALLENGE 2024

MATI SUPER BRANDS LIMITED YADHAMINI MASHINDANO YA WEST KILI TOUR CHALLENGE 2024

Ferdinand Shayo ,Kilimanjaro.

 
Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited imedhamini mashindano ya mbio za riadha,baiskeli na piki piki ya West Kili Challenge 2024 yaliyoafanyika katikati ya Hifadhi ya Misitu ya West Kilimanjaro na kukutanisha mamia ya Wanamichezo kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania .
 
Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya Mati Super Brands Limited mkoa wa Kilimanjaro Brayson Mnene amesema kuwa wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza utalii wa michezo na uhifadhi wa misitu .

Grayson amesema kuwa Mari Super Brands Limited ni wadau wa maendeleo na wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kukuza michezo mbali mbali ikiwemo riadha,piki piki na baiskeli.

 
Mratibu wa Shindano ya West Kili Tour Challannge Mensiaur Elly amesema mashindano hayo yanalenga kutoa fursa kwa watu mbali mbali kupata fursa ya kufanya michezo katikakati ya misitu wa hifadhi ya Shamba la West Kilimanjaro na kujionea vivutio mbali mbali ikiwemo wanyamapori,maporomoto yam aji na miti ya asili.
 
Mkuu wa Wilaya ya Siha Christopher Timbuka amesema mashindano hayo yamehuduriwa na mamia ya wananchi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro ambao wamepata fursa ya kufanya michezo na utalii wa ndani kwa Pamoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here