Home LOCAL BRELA YATAJA VIGEZO KUSAJILI KAMPUNI 

BRELA YATAJA VIGEZO KUSAJILI KAMPUNI 

Sheria ya kampuni sura ya 212, ilianzishwa ambapo lengo lilikuwa ni kuweka mfumo kisasa, kisheria kwa ajili ya uanzishwaji, usimamizi na uendelezaji kampuni Nchini hivyo basi Brela ambayo ndio msimamizi usajili kampuni imetoa vigezo vya kufanya usajili huo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Juni 20,2024 Mkurugenzi wa Kampuni na majina ya Biashara kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Lameck Nyangi,  amesema usajili wa Kampuni, Kurugenzi ya Kampuni na Majina ya Biashara   mtu kuanzia mmoja au wa wawili ambao wanataka kusajili kampuni yao wanatakiwa kuwa na taarifa za msingi ambazo wanatakiwa kujaza katika fomu ambayo inapatikana kwenye tovuti ya BRELA.
Amesema taarifa hizo ni pamoja na Mkurugenzi, Namba ya Nida, Namba ya mlipa Kodi (Tin namba),Anuani ya makazi ya Wakurugenzi kwa Watanzania na kwa wageni taarifa zinazohitakika ni pamoja na Hati ya kusafiria,Namba ya utambulisho ya mlipa Kodi (Tin namba) kwa wakurugenzi, Jina la Kampuni lilipendekezwa.
Akitaja kiwango Cha   ada za usajili wa kampuni mpya kuwa  zinaanzia  kwa Sh.20,000, Sh. 1000,000, Sh. 5,000,000, Sh.20,000,000 mpaka Sh.50,000,000 na kwamba viwango hivyo ni kutokana na mtaji wa kampuni husika na kwa usajili wa kampuni za kigeni gharama za usajili ni Dola za Marekani 1,190,Filing fee ni Sh.66,000 na Stamp Duty 6,200.
Aidha amesema Sheria ya usajili wa kampuni katika kifungu cha nne mpaka cha tisa kimeeleza namna gani mkataba wa kampuni au kanuni za uendeshaji unatakiwa kuandaliwa. Hata hivyo taratibu za usajili wa kampuni , kuna mabadiliko yaliyotokea ambayo yalisababisha matumizi ya mtandao na BRELA kuanzia mwaka mwaka 2018 ilitambulisha mfumo wa kusajili kampuni kwa njia ya mtandao.
“Usajili wa kampuni unafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni ya Tanzania ya mwaka 2002 ambayo ilikuwa haina tofauti na Sheria ya 1932 ambayo chimbuko lake ni Sheria ya Kingereza ya mwaka 1929 lakini chimbuko halisi la sheria imetokana na kampuni za India mwaka 1913 sheria zote mbili zinamchango mkubwa kwa sheria ya kampuni ya Tanzania ya mwaka 1932.Kuna mfanano wa vifungu vingi ambavyo vimeletwa katika sheria ya kampuni nchini Tanzania”, amesema Nyangi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here