Home BUSINESS WIZARA YA FEDHA YAWASHAURI WASTAAFU KUJIHEPUSHA NA MATAPELI

WIZARA YA FEDHA YAWASHAURI WASTAAFU KUJIHEPUSHA NA MATAPELI

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini wizara ya fedha Benny Mwaipaja wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari za mitandaoni Mkoani Morogoro.

MOROGORO 

Wizara ya Fedha imewashauri wastaafu wote kujiepusha na matapeli wanaowapigia simu kutaka fedha na kuwalaghai kwamba watawasaidia kupata mafao yao kwa haraka, na kwamba Wizara haina utaratibu huo.

Wizara ya Fedha imeendelea kuwakumbusha wastaafu kutojihusisha na utoaji wa fedha zozote kwa mtu au watu kwa kigezo cha kusaidiwa kupata PENSHENI,kwani wizara hiyo haiombi fedha ili kuwasaidia wastaafu.

Hayo yameelezwa leo Mei 13,2024 Mkoani Morogoro na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini wizara ya fedha Benny Mwaipaja wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari za mitandaoni huku akiwaomba pia kuwa mstari wa mbele katika kukumbushia suala hilo.

“Lengo la kufanya haya ni kutaka kuwasaidia wastaafu hawa na familia zao wasiendelee kutapeliwa kwani kwasasa haya matukio yamekuwa yakiongezeka unakuta mtu kakaa zake mezani anapiga simu kuomba fedha kwa mstaafu ili amtumie help amsaidie kwahiyo naamini kupitia kwenu hawa watu tutaweza kuwasaidia,”amesema.

Aidha amesema kuwa wanahabari ni muhimu sana kuwashirikisha katika suala hilo kutokana na namna ambavyo teknolojia inazidi kukuwa zaidi na wahalifu wanabuni njia za kutaka kuwatapeli wastaafu.

Kwa upande wake Mwenyejiti wa mafunzo hayo Mathias Canal ameipongeza Wizara ya fedha kwa kuandaa mafunzo hayo yenye lengo la kuwaongezea uzoefu wanahabari haonl pamoja na kuwasaidia wastaafu kuepukana na changamoto wanazozipitia kipindi cha kudai pensheni zao.

Previous articleKAMATI KUU CHADEMA  YAFANYA USAILI WA WAGOMBEA WA UONGOZI 
Next articleMEJA JENERALI MABELE AIPONGEZA SERIKALI KUWEKEZA KWA VIJANA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here