Home BUSINESS UFARANSA NA TANZANIA KUIMARISHA BIASHARA

UFARANSA NA TANZANIA KUIMARISHA BIASHARA

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui, akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Ali Mwadini akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake katika mkutano huo uliofanyika kwenye makazi ya Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Jijini Dar es Salaam.

(Picha na: Hughes Dugilo)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

UJUMBE wa wafanyabiashara kutoka kampuni 27 za Ufaransa umeahidi kushirikiana na wafanyabiasha wa Tanzania katika kukuza biashara na fursa za uwekezaji.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika makazi ya ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania , rais wa Chemba ya Biashara ya Ufaransa na Tanzania (FTCC), Christopher Darmois amesema ushirikiano huo utaongeza wigo wa Kibiashara baina ya nchi hizo mbili, nakwamba utakuwa endelevu.

“Tunafuraha kushuhudia muunganiko wa makampuni ya Biashara ya Ufaransa na Tanzania, na kustawisha mazingira ya kiubunifu ya Biashara.

“Jukwaa hili bila shaka litafungua njia ya kuongezeka kwa Biashara na uwekezaji utakaonufaisha nchi zetu mbili” amesema Darmois.

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui, amesema kuwa Ufaransa na Tanzania zina urafiki wa muda mrefu na kusisitiza kuwa kuwepo kwa mashirikiano hayo ya Kibiashara kutaendeleza kuimarisha uhusiano uliopo.

“Jukwaa hili linaonesha dhamira ya kuimarisha uhusiano wa pande zote mbili kati ya mataifa yetu haya mawili.

“Kupitia Jukwaa hili inaonesha dhamira yetu ya kuimarisha uhusiano wa Kibiashara. Kupitia juhudi za ushirikiano, tunaweza kuendeleza maendeleo endelevu na kuunda manufaa ya kudumu ya kiuchumi kwa nchi zetu zote mbili” amesema Balozi Hajlaoui.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Ali Mwadini amesema Tanzania imewakikishia wafanyabiasha hao kuwa Tanzania ni mahali sahihi pa kufanya Biashara na uwekezaji, na kwamba ina rasilimali nyingi kwenye maeneo mbalimbali na miundombinu imara inayounganisha mipaka ya nchi mbalimbali inazopakana nazo.

“Nipende kuwahakikishia kuwa nchi yetu ina mazingira mazuri ya Biashara na uwekezaji, ni nchi kubwa na imepakana na nchi jirani takribani kumi zikiwemo tunazopakana nazo kwenye bahari ya indi.

” Hivyo zipo sababu nyingi za kuwa na mashirikiano ya Biashara na Kampuni hizi kutoka Ufaransa” amesema Mwadini.

Chemba ya Biashara ya Ufaransa na Tanzania, (FTCC), ilianzishwa mwaka 2019, ni Shirika la Kimataifa lisilo la faida lenye wanachama wafanyabiasha 118 kutoa Ufaransa katika nchi 93 Duniani.

Aidha FTCC inatoa fursa kwa wafanyabiashara na makampuni kuyafikia masoko na kujenga uhusiano wa kudumu Kibiashara kwaajili ya maendeleo yenye ufanisi wa Kibiashara.

FTCC pia imejitolea kusaidia makampuni na wafanyabiasha wa ufaransa waliopo Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kukuza mahusiano na fursa za Kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania.

Previous articleMATUMIZI YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU ZINASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI NA KIJAMII
Next articleRAIS SAMIA AKIONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU CHAMWINO DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here