Home BUSINESS MATUMIZI YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU ZINASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI NA...

MATUMIZI YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU ZINASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI NA KIJAMII

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ni sehemu ya mikakati ya serikali katika kuongeza hamasa ya kukuza elimu ujuzi na ubunifu katika kuchangiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

 

Mkenda amesema hayo Mei 27, 2024 jijini Tanga wakati akifungua Maadhimisho hayo ambapo amesema matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu ni nyenzo zinazosaidia kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii pamoja na kuchagiza maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.

‘’Serikali inatambua umuhimu na mchango mkubwa wa elimu, ujuzi na ubunifu katika kuchagiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii na imepiga hatua kufikia malengo ya Mipango na Mikakati mbalimbali ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa, ikiwemo Dira ya Taifa 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, Sera ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023; Ajenda 2063: The Africa We Want; Malengo ya Maendeleo Endelevu-2030, alieleza Waziri Mkenda.

Aidha amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu, ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa miundombinu, sambamba na kuanza utekelezaji wa Sera ya elimu na mitaala iliyobreshwa pamoja na kuendelea ujuzi na ubunifu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Elimu, Michezo na Utamaduni Mhe. Husna Sekiboko amesema Bunge la Tanzania linatamani kuona bunifu zinazoibuliwa hazibaki kwenye Maonesho, badala yake ziendelezwe na kufikia hatua ya kubiasharishwa ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kutoa hamasa kwa Wabunifu mbalimbali.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Dkt. Baltida Burian ameshukuru kuufanya mkoa huo Mwenyeji wa Maadhimisho na kwamba ni heshima kubwa kwa Wanatanga wote na kuwataka kutumia fursa hiyo kikamilifu kutembelea maonesho hayo kujifunza juu ya teknolojia mbalimbali.

Previous articleTBA YAGEUKA KIVUTIO MAONESHO YA SEKTA YA UJENZI BUNGENI DODOMA
Next articleUFARANSA NA TANZANIA KUIMARISHA BIASHARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here