Home LOCAL KAMISHNA KYANDO: WASIOLIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KUWAJIBISHWA

KAMISHNA KYANDO: WASIOLIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KUWAJIBISHWA

Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, Shukrani Kyando, akizungumza katika Mkutano na waandishi wa Habari Mei 11, 2024, Jijini Dar es Salaam, kuhusu hatua walizochukua katika kutekeleza agizo la Waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa la kutoa siku 30 kwa wadaiwa wote wa kodi ya pango la Ardhi kulipa kodi hiyo.

Afisa Ardhi Mwandamizi Kitengo cha Kodi Dar es Salaam na Pwani, Seif Mahiza, akielezea namna kitengo hicho kilivyojipanga kuwahudumia wananchi wakati wa zoezi la kukusanya Kodi hiyo.

DAR ES SALAAM

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, Shukuran Kyando amewataka Wananchi kuwajibika kulipa kodi ya pango la Ardhi kabla ya tarehe 1 Julai mwaka huu ili kuepuka kuwajibishwa kisheria kwa kupelekwa Mahakamani

Aidha, amezielekeza Halmashauri zote katika mikoa hiyo kuongeza ufanisi kwa kuongeza muda wa kazi kuanzia saa mbili subuhi hadi saa mbili usiku, ili kutoa fursa kwa wananchi wengi kupata muda wa kutosha wa kulipa kodi zao za Ardhi na pango.

Kamishna Kyando ametoa maelekezo hayo Mei 11, 2024 kwenye mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja baada ya Waziri mwenye dhamana katika Sekta ya Ardhi Jerry Silaa kutoa agizo la kutoa siku 30 kwa wadaiwa wote wa kodi ya pango na Ardhi kulipa kodi hiyo.

Amesema kuwa suala la ulipaji kodi ya Ardhi ni la Kisheria, na kwamba kila mmiliki anapaswa kuilipa kwa mujibu wa Sheria.

“Kila Miliki wa Ardhi anapaswa kulipa kodi ya pango na Ardhi kwa mkupuo au kwa awamu katika mwaka.

“Sasa ni muda muafaka kwa wamiliki wa Ardhi Dar es Salaam na Pwani kulipa kodi zao kwa wakati uliotajwa ili kuepuka usumbufu wa kisheria” amesema Kyando.

Amefafanua kuwa kwa wale wote watakaokiuka maagizo hayo watachukuliwa hatua stahiki ikiwemo kufikishwa Mahakamani na Ardhi zao kumilikishwa wengine au kuuzwa.

Naye, Afisa Ardhi Mwandamizi Kitengo cha Kodi Dar es Salaam na Pwani, Seif Mahiza, amesema Wizara imeweka mazingira wezeshi na rafiki kwa wananchi kulipa kodi zao, ambapo wanaweza kulipa kupitia simu zao za mkononi kwa kutumia namba maalum ya malipo (Control number), na kwamba hatua hiyo itawaondolea usumbufu.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kwa wale wote ambao watashindwa kutumia njia ya mtandao, wanaweza kupata huduma hiyo katika Ofisi za Wizara zilizopo Magogoni Jijini Dar es Salaam.

Previous articleSERIKALI YAPONGEZA MCHANGO WA RED CROSS TANZANIA
Next articleBALOZI NCHIMBI ASHIRIKI MISA, SHEREHE KUWEKWA WAKFU ASKOFU MSAIDIZI KIBOZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here