Home LOCAL WADAU WAHIMIZWA KUHAMASISHA UMUHIMU WA LISHE BORA

WADAU WAHIMIZWA KUHAMASISHA UMUHIMU WA LISHE BORA

Halmashauri ya Jiji la Mbeya imewasihi wadau na taasisi mbalimbali kujikita katika kuelimisha jamii juu ya lishe bora na mifumo ya chakula lengo likiwa ni kuendeleza mapambano dhidi ya udumavu Jijini Mbeya.

Akizungumza kwenye warsha ya kujadili masuala ya lishe, leo Aprili 3, 2024 katika hoteli ya Usungilo jijini Mbeya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bw.John Nchimbi amesema kuna kila sababu ya kujikita katika kutoa elimu, kubuni mbinu zitakazowezesha na kuhamaisha jamii kuzingatia lishe bora.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa watoto wakipata lishe bora itawawezesha kuwa na afya bora kiakili na kimwili hivyo kuwa wabunifu na wavumbuzi na hatimaye kujenga taifa lenye wataalam watakaoweza kusimamia vyema maslahi na maendeleo ya nchi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji la Mbeya, Dkt. Yesaya Mwasubila amesema kuwa hali ya lishe Jijini Mbeya kwasasa sio mbaya na amewapongeza walimu kwa kuthubutu wa kuzungumza na wazazi juu ya uchangiaji wa huduma ya utoaji chakula shuleni pamoja na kutaka itungwe sheria ndogo itakayowabana wazazi kuchangia chakula. 

Naye Bi.Itika Mlagalila, Afisa lishe Jiji la Mbeya, amebainisha athari zinazoweza kujitokeza iwapo jamiii itakosa lishe bora kuwa ni pamoja na kushuka kwa kiwango cha uzalishaji mali, kwakuwa jamii itakuwa inajiuguza badala ya kufanya shughuli za uzalishaji, uwezo wa mtoto kuelewa awapo shuleni kuwa mdogo kutokana na kukosa viini lishe, hivyo ni muhimu mama mjamzito kuzingatia lishe katika siku 1000 ujauzito mpaka mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili.

Aidha Bi.Judith Sarapion kutoka Shirika la Helvets ambalo ni muwezeshaji wa Mifumo ya Chakula Jijini Mbeya, amesisitiza kuzingatia utoaji wa elimu ya lishe kwa makundi yote kuanzia watu wazima,watoto waliopo shuleni na vijana ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu elimu ya lishe na kunufaika na lishe sambamba na kujenga kizazi kijacho chenye afya bora.

Mwalimu Bether Gerald kutoka Idara ya Elimu ya Msingi Jiji la Mbeya ameeleza kuwa miongozo imeeleza bayana kuwa ni wajibu wa mzazi kuchangia chakula pia ni haki ya mtoto kupata chakula akiwa shuleni.

Mpaka. sasa asilimia 44.8 ya wanafunzi wa shule za sekondari za Serikali wanapata chakula shuleni baada ya wazazi wao kuchangia chakula, hivyo ameiomba Halmashauri kuendelea kuweka mkazo kwenye sheria ndogo ili kuwabana wazazi na kuwakumbusha kuwa kuchangia chakula shuleni ni lazima na sio hiari.

Mkakati huu wa wa lishe ni muendelezo wa jitihada za Halamshauri ya Jiji la Mbeya kwa kushirikiana na wadau kuhakikisha jamii inaondokana na mitazamo hasi juu ya uchangiaji wa huduma ya utoaji chakula shuleni.

Previous articleMONGELLA AKABIDHIWA ‘MIKOBA’ RASMI YA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA
Next articleTANESCO YAWAPA TABASAMU WATOTO WA KITUO CHA NEW FARAJA MBURAHATI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here