Home LOCAL TAWLA YAJIPANGA KUTOA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA MAKUNDI MAALUM NA...

TAWLA YAJIPANGA KUTOA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA MAKUNDI MAALUM NA WANAWAKE

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TAWLA, Lulu Ngw’wanakilala akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) uliofanyika kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam,

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Bi. Tike Mwambipile mkutano mkuu wa mwaka wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) uliofanyika kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es SalaamSalaam.

Tom Nyanduga Kamishna Mstaafu wa Haki za binadamu na Utawala Bora Tume ya Haki za Binadamu akiwasilisha mada kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wanasheria Wanawake uliofanyika kwenye hoteli ya New Afrika Aprili 20′ 2024.

Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo kushoto ni Balozi Mwanaidi Maajal na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania Joaquine De Mello. 

…………………

NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM

Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kimejipanga kuendelea kutoa elimu kwa makundi maalamu ikiwemo wanawake ili kuhakikisha inakabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi ambazo zimekuwa zikileta madhara makubwa katika jamii.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam kando ya mkutano mkuu wa mwaka wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) uliofanyika kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TAWLA, Lulu Ngw’wanakilala, amesema kuwa wakati umefika wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuleta tija kwa Taifa.

Ngw’wanakilala amesema kuwa upatikanaji wa haki kwa wanawake umekuwa ukiwaathiri kwa kiasi kikubwa katika jamii.

“Mabadiliko ya tabia ya nchi imekuwa ikiwaathiri wanawake kutokana na changamoto zinajitokeza ikiwemo mafuriko” amesema Ngw’wanakilala.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Bi. Tike Mwambipile
amesema kuwa wamejipanga kuwekeza nguvu katika kupinga ukatili wa kijinsia unaofanywa na baadhi ya watu wenye nia mbaya.

Ngw’wanakilala amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuwasema vibaya viongozi wa nchi kuwa kutumia lugha ambazo sio rafiki kwa jamii.

“Sheria zetu za nchi zinaelekeza unapomtukana mtu ni kosa la jinai na madai, tunatumia fursa hii kukemea na kuhamasisha jamii kutumia mitandao ya kijamii vizuri katika kuhabarisha na kuelimishana na kupekana na makosa ya kimtandao”

Kauli mbiu ya mwaka huu katika mkutano mkuu : athari ya mabadiliko ya tabia ya nchi kwa wanawake nini kinawathiri zaidi.

Previous articleMSAJILI WA HAZINA AZUNGUMZA NA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI YA PERSEUS
Next articleWAZIRI MKUU AWAAGA VIONGOZI WA DINI, UZINDUZI WA ROUTE YA SGR DAR – DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here