Home LOCAL SERIKALI YA Dkt. SAMIA IMEENDELEA KUSIMAMIA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI – Prof....

SERIKALI YA Dkt. SAMIA IMEENDELEA KUSIMAMIA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI – Prof. BUSAGALA 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Profesa Lazaro Busagala, akizungumza na Wahariri na Waandishi wakati wa kikao kazi cha Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR) na kufanyika jijini Dar es Salaan leo Aprili 29, 2024.

Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, akizungumza katika mkutano huo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Peter Ngamilo,  akifafanua jambo wakati wa kikao kazi cha Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR) jijini Dar es Salaan leo Aprili 29, 2024.

Baadhi ya Wahariri wakifuatilia mkutano huo.

DAR ES SALAAM 

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea na juhudi za kusimamia udhibiti wa matumizi salama ya mionzi ili kuepuka madhara yake.

Hayo yamebainishwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Profesa Lazaro Busagala, katika kikao kazi na Wahariri wa Habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, kilichofanyika leo Aprili 29, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita kupitia TAEC imeendelea na juhudi za kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyukilia nchini, ambapo juhudi kubwa kuhakikisha wananchi wanaelewa fursa zilizopo katika matumizi salama ya sayansi ya nyuklia kwa ajili ya kujilitea maendeleo.

Aidha, Profesa Busagala amesema kuwa, TAEC imeongeza program za kujitangaza kutoka 12 hadi 60 kwenye televisheni, redio, magazeti, mitandao ya kijamii na kushiriki katika maonesho mbalimbali.

“Vifaa vya kisayansi ni nguzo muhimu katika kudhibiti athari za mionzi, tafiti, usimamizi na uendelezaji wa Teknolojia ya Nyuklia, hivyo Serikali ya Awamu ya Sita, inaendelea kuweka bajeti na kununua vifaa, vyenye jumla ya shilingi bilioni 2.9  vinaendelea kununuliwa.

“Serikali ya Mheshimwa Rais Samia, imefanikiwa kuongeza tengeo la bajeti ya utafiti kwa TAEC hadi kufikia shilingi milioni 450 katika mwaka wa fedha 2023/2024, juhudi hizo zimefanyika ili kupata fursa zaidi za sayansi na teknolojia ya nyukilia na pia kuwalinda wananchi na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi” amesema Prof. Busagala.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa katika juhudi hizo za Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka mitatu machapisho zaidi ya 25 ya kitafiti yamepatikana katika juhudi hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here