Home BUSINESS MKUTANO MKUU WA ALAT 2024; WAZIRI MCHENGERWA ATEMBELEA BANDA LA PSSSF

MKUTANO MKUU WA ALAT 2024; WAZIRI MCHENGERWA ATEMBELEA BANDA LA PSSSF

ZANZIBAR

MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma umeshiriki kwenye Mkutano Mkuu wa 38
wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa Tanzania (ALAT) uliofanyika jijini  Zanzibar na kupata fursa ya kuelimisha
kupitia maonesho na uwasilishaji wa mada kwa wajumbe wa mkutano Mkuu.

Mkutano
huo muhimu hujumuisha Wenyeviti wa Mikoa na Halmashauri zote nchini,
Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa zote nchini, Mameya, na Wajumbe wa
Kamati Tendaji ya ALAT.

Meneja
wa Ofisi ya Zanzibar wa PSSSF, Bi. Amina Kassim aliwaeleza wajumbe wa mkutano
huo kuhusu maboresho ya kidijitali yaliyofanywa na PSSSF ili kuboresha huduma
kwa wateja ikiwemo kuhusu mfumo mpya wa kupokea madai ya mafao mtandaoni na usajili
wa wanachama mtandaoni.

Aidha
aliwaomba waendelee kutoa ushirkiano ili kutatua changamoto za kiutendaji kwa
wakati.

Mkutano
huo ulifunguliwa rasmi na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa na
kufungwa na Waziri wa Nchi Ofisi yanRais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohamed.

Mkutano
Mkuu umehudhuriwa na  wajumbe na taasisi
wadhamini takribani 450.

 

 

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here