Home BUSINESS BOT, WIZARA YA ELIMU KUPELEKA ELIMU YA FEDHA VYUONI

BOT, WIZARA YA ELIMU KUPELEKA ELIMU YA FEDHA VYUONI

Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga, akizungumza alipokuwa akifungua Warsha ya siku tatu kuhusu umuhimu wa uwepo wa elimu ya fedha kwenye mtaala wa elimu ya juu, Aprili 17,2024 Jijini Dar es Salaam

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),  Sauda Msemo akitoa hotuba ya utangulizi wakati wa ufunguzi wa Warsha hiyo, Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imejipanga kutoa elimu ya fedha kwa wanafunzi wa Elimu ya juu walioko katika vyuo mbalimbali, ili kuwaandaa vijana kuwa na nidhamu ya fedha.

Hayo yameelezwa Aprili 17,2024 Jijini Dar es Salaam, na Naibu Gavana wa BoT, Sauda Msemo wakati akiwasilisha taarifa yake katika Warsha maalum ya siku tatu kuhusu umuhimu wa uwepo wa elimu ya fedha kwenye mtaala wa elimu ya juu kwa wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo viongozi wa taasisi za elimu ya juu nchini.

Amesema kuwa mwezi April mwaka jana, BoT iliwashirikisha wakuu wa taasisi za Elimu ya Juu nchini, kwa uwakilishi wa wakuu wa vyuo vikuu pamoja na TCU na NACTIVET kwa lengo la kukubaliana juu ya azma ya kufundisha somo la elimu ya fedha ngazi ya elimu ya juu nchini.

Hadi hivi sasa taasisi tatu za elimu ya juu zimechukua hatua za kuingiza somo la elimu ya fedha katika mitaala yao, hivyo warsha hii ni kuchochea uwepo wa elimu ya fedha kwa vyuo vingi nchini kuendana na mabadiliko ya mageuzi ya kiuchumi nchini,”amesema Msemo.

Ameongeza kuwa takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022 inaonesha takribani watu asilimia 34.5 ni vijana walio na umri kati ya miaka 15-35 hivyo ili kuleta tija na ufanisi katika masuala ya uchumi ujuzi na uzoefu wa masuala ya fedha ni moja ya sifa muhimu katika kufikia azma hiyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akizungumza alipokuwa akifungua Warsha hiyo, amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kujenga uelewa wa masuala ya fedha kwa wananchi wa kada mbalimbali wakiwemo wanafunzi, ili kukuza uelewa kwa jamii kuhusu nidhamu ya fedha.

“Wizara tutahakikisha elimu ya fedha inafundishwa katika mfumo wa elimu nchini, hivyo twende kwa haraka kuhakikisha vijana ambao ni sehemu ya jamii wanakuwa na uelewa wa masuala ya fedha, hivyo natarajia wakuu wa vyuo mtabeba uelewa huo muhimu kwa vyuo vyetu nchini.

“Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ipatiwe taarifa ya tathmnini mtakazofanya ili itusaidie katika kufanya maamuzi, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kujenga uelewa wa masuala ya fedha kwa jamii,” amesema Kipanga.

Previous articleU.S. CDC NA THPS WAKABIDHI JENGO LA KLINIKI YA TIBA NA MATUNZO NA VIFAA TIBA VYA MILIONI 270 KIGOMA
Next articleSOMA MAGAZETI YA LEO APRILI 18-2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here