Home LOCAL UBALOZI WA USWISI, AMEND WAENDELEA KUTOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI,HUDUMA YA KWANZA...

UBALOZI WA USWISI, AMEND WAENDELEA KUTOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI,HUDUMA YA KWANZA KWA MADEREVA BODABODA JIJINI TANGA

Na: Mwandishi Wetu,Tanga

UBALOZI wa Uswisi nchini Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya AMEND wameendelea kutoa elimu ya usalama barabarani ikiwemo elimu ya huduma ya kwanza kwa madereva bodaboda, lengo likiwa kuwasaidia madereva hao kuwa na uwezo wa kutoa msaada pindi ajali zinapotokea.

Wakizungumza baada ya kupatiwa mafunzo hayo baadhi ya madereva bodaboda wamesema elimu waliyoipata kuhusu usalama barabarani itawasaidia kuendesha kwa tahadhari pindi wanapokuwa barabarani na hivyo kuepusha ajali ambazo zimekuwa zikisababisha video na ulemavu wa kudumu.

Dereva bodaboda katika kituo cha Mikanjuni hospitali Ally Zuberi na Faky Hamis wamefafanua kwamba ukosefu wa elimu umekuwa chanzo kikubwa cha ajali za barabarani kwa madereva wengi wa bodaboda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodaboda Kituo cha Mikanjuni Hospitali Mwin’dadi amesema kwamba kutozitambua sheria na alama za barabarani imekua ndio sababu ya ajali ya nyingi kutokea huku akibainisha elimu waliyoipata itawasaidia kujiepusha dhidi ya ajali.

“Tunawashukuru AMEND na Ubalozi wa Uswisi kwa kutambua kundi hili la usafirishaji kwa kutumia bodaboda,mafunzo ambayo tumeyapata yametuongezea uelewa kuhusu matumizi sahihi ya sheria za usalama barabarani lakini wakati huo kuwa na uelewa wa kutoa huduma ya kwanza kwa dereva au abiria atakeyapata ajali.”

Ameongeza watakuwa mstari wa mbele kutoa msaada pale ajali itakapotokea ambapo wameendelea kusema kuwa elimu hiyo watawashirikisha na madereva wenzao ili kushiriki katika utoaji wa huduma.

Wakati huo huo Ofisa Miradi wa AMEND
Ramadhani Nyanza amesema elimu ya huduma ya kwanza waliyoitoa kwa madereva bodaboda imeleta mwanga kwa madereva hao kwa kujua namna bora ya kutoa msaada pale kunapotokea ajali.

Nyanza amesema mpaka sasa madereva bodaboda takribani 126 katika Jiji la Tanga wamefikiwa kwa kupatiwa elimu ambapo amebainisha malengo ni kuwafikia madereva 500 kwa mkoa Tanga.

Awali Benilda Mtumbuka ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii kata ya Magaoni ametoa shukrani kwa Ubalozi wa Uswisi na taasisi ya AMEND kutokana na elimu ya usalama barabarani kwa madereva bodaboda.

Mwisho

Previous articleDkt. NCHIMBI AKISALIMIANA NA DIAMOND MSIBANI KWA MZEE RUKSA
Next articleWATENDAJI HALMAHAURI YA MSALALA WATAKIWA KUA WAADILIFU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here