Home BUSINESS TANZANIA NA HUNGRY KUSHIRIKIANA KATIKA USAFIRI WA ANGA

TANZANIA NA HUNGRY KUSHIRIKIANA KATIKA USAFIRI WA ANGA

Dar es Salaam.

Serikali ya Tanzania na serikali ya Hungary wametiliana saini mkataba katika usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili ili na kuanzisha safari za moja kwa moja Kutoka Hungry kuja nchini kwa lengo la kukuza utalii.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania , January Makamba, amesema kuwa hivi karibuni Tanzania imeshuhudia wimbi la watalii kutoka Hungary wanaotembelea nchini na kwamba kwa miaka miwili iliyopita watalii walikuwa 5000 na mwaka Jana watalii waliongezeka hadi 1000.

Makubaliano hayo yamefanyika katika ya Waziri huyo kwa upande wa Tanzania, na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Péter Szijjártó.

“Tumezungumza kuhusu utalii kwamba Tanzania Ina vivutio vingi na Hungary ni chanzo Cha watalii Tanzania, tumeshuhudia ukuaji wa wimbi la watu kutoka hungry wanaokuja Tanzania kutalii, miaka miwili iliyopita walikuwa 5000 na mwaka Jana ni 1000 hivyo kuna ongezeko kubwa lakini pia kuna fursa kubwa kutokana na ongezeko hilo”

“Jambo hilo litawezeshwa kama kutakua na usafiri wa Moja kwa moja wa anga kutoka hungary mpaka Tanzania, kwa msingi huo, tumekubaliana kwamba tutasaini mkataba wa usafiri wa anga kati ya nchi zetu mbili ili kuwezesha ndege zisafiri Moja kwa Moja kutoka hungary kuja hapa kwasababu hilo lutawezesha watalii wengi kuja zaidi na kutembeleana zaidi na biashara kuongezeka” Amesema Waziri Makamba.

Aidha amesema kuwa katika mazungumzo yao, wamekubaliana kufanyika kwa makongamano ya biashara kati ya nchi hizo mbili, kufanya ziara za kibiashara kati ya Sekta binafsi ya Tanzania kwenda hungary na Sekta binafsi ya hungary kuja hapa ili fursa ziweze kuonekana na biashara iweze kukua.

Katika suala la Elimu, Makamba alisema wamekubaliana waharakishe utekelezaji wa kupeana scholarship kila mwaka ambapo Tanzania wameomba fursa hizo ziongezwe na zipanuke zaidi.

“Tumezungumzia suala la ushirikiano katika elimu na kwa miaka mingi hungary imekuwa sehemu ambapo watanzania wanasoma, wenzetu mwaka 2018 walianzisha programu ya scholarship na tangu wakati huo watanzania vijana karibu 146 wamenufaika na scholarship hizo na Kila mwaka tunapeleka vijana kule”

“Mwaka Jana alivyokuja Rais wao hapa, yalifanyika makubaliano ya scholarship zaidi ya 30 kila mwaka lakini na sisi tukawapa scholarship Tano Kila mwaka, tumekubaliana sasa tuharakishe utekelezaji wa makubaliano yale na tumeomba kwamba fursa hizo ziongezwe na zipanuke zaidi” Alisema Waziri Makamba.

Previous articleKAMATI YA PIC YARIDHISHWA NA UWEKEZAJI WA JENGO LA PSSSF COMMERCIAL COMPLEX
Next articleSOMA MAGAZETI YA LEO MACHI 29-2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here