Home LOCAL RAIS SAMIA AWATAKA WATANZANIA KUYAISHI MAISHA YA HAYATI MWINYI

RAIS SAMIA AWATAKA WATANZANIA KUYAISHI MAISHA YA HAYATI MWINYI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema ataendelea kuyaenzi maono ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Hayati Ali Hassan Mwinyi kwa kusimamia ustawi wa wananchi, kutenda haki na kuwa mstahamilivu.

Rais Samia amesema hayo katika mazishi ya kitaifa ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Hayati Ali Hassan Mwinyi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Amani Abeid Karume.

Aidha, Rais Samia amesema kwa ustahamilivu wake wakati wa uongozi, hayati Mwinyi aliheshimu haki za binadamu na utawala bora na kuruhusu maoni tofauti yenye kuikosoa serikali.

Vile vile, Rais Samia amesema licha ya Hayati Mwinyi kuwa kiongozi katika vipindi vigumu kisiasa na kiuchumi aliweza kuhakikisha utulivu na kufanya mageuzi makubwa katika nyanja za kisiasa na kiuchumi.

Rais Samia pia amesema Hayati Mwinyi ana mchango endelevu uliozisaidia serikali za awamu zilizofuatia kwani ndiye aliyehamasisha uwekezaji kutoka sekta binafsi na soko huria zilizochangia katika ukusanyaji mapato.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka Watanzania kuishi kwa kufuata misingi bora ya maisha na malezi na kuyachukulia maisha ya Hayati Mwinyi kama funzo katika kuwalea vijana kwa kuzingatia maadili ya dini na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Hayati Mwinyi ameacha alama za kudumu na za kihstoria kama Rais wa mwisho kuiongoza Tanzania katika mfumo wa chama kimoja na kuweka ukomo wa mihula ya Urais.

Zuhura Yunus,

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Previous articleRAIS SAMIA AONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI WA ZANZIBAR  KUAGA MWILI WA RAIS MSTAAFU MZEE ALI HASSAN MWINYI UWANJA WA AMANI ZANZIBAR
Next articleDkt. NCHIMBI AKISALIMIANA NA DIAMOND MSIBANI KWA MZEE RUKSA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here