Home INTERNATIONAL POSCO YADHAMIRIA KUONGEZA UWEKEZAJI TANZANIA

POSCO YADHAMIRIA KUONGEZA UWEKEZAJI TANZANIA

Seoul, Korea Kusini

Katika hatua ya kuongeza Uwekezaji na kuimarisha ushirikiano wa biashara kimataifa Kampuni ya kimataifa inajishughulisha na uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na madini ya chuma ijulikanayo kama POSCO yenye makao makuu yake nchini Korea Kusini, imedhamiria kuongeza uwekezaji katika sekta ya madini nchini Tanzania.

Hayo yamebainishwa katika mkutano wa Madini Muhimu na Mkakati kwa Bara la Asia na Afrika wakati wa uwasilishaji mada juu ya jiolojia ya Tanzania kwa Taasisi ya Jiosayansi na Madini ya nchini Korea Kusini (KIGAM) uliofanyika jijini Seoul nchini Korea Kusini.

Katika Mkutano huo Kampuni ya Kimataifa ya POSCO iliueleza ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo kuwa wamedhamiria kuongeza uwekezaji nchini Tanzania hususani kwenye bidhaa zinazotengenezwa kwa kutumia Madini Muhimu na ya Mkakati.

Kampuni ya POSCO ilieleza kuwa kwasasa wameingia ubia na kampuni ya uchimbaji madini ya Black Rock ambayo ina ubia na Serikali ya Tanzania kwenye mradi wa uchimbaji wa madini ya Kinywe wilayani Mahenge yaani _Mahenge Graphite Mine._

Kwa upande wake , Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo aliihakikishia kampuni ya POSCO kuwa Serikali ya Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha na wa kila namna itakapohitajika kwasababu sekta ya madini Tanzania inahitaji wawekezaji makini na wenye uzoefu kama kampuni ya POSCO.

Sambamba na mkutano huo ujumbe wa Tanzania ulipata fursa ya kutembelea maonesho ya kimataifa ya Korea yajulikanayo kama EV TREND KOREA kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni ya POSCO.

Previous articleRAIS SAMIA HATAKI MISUKOSUKO KWA WAFANYABIASHARA- DKT. BITEKO
Next articleMIGODI YA BARRICK BULYANHULU NA NORTH MARA ILIVYOSHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here