Home BUSINESS MTANZANIA SIMON MNKONDYA APELEKA KILIMO CHA VANILLA KENYA

MTANZANIA SIMON MNKONDYA APELEKA KILIMO CHA VANILLA KENYA

 
Mkurugenzi wa Vanilla International Limited wa Tanzania ameweza kufanikiwa kuanzisha mashamba ya Vanilla katika eneo la Kaunti ya Kilith Nchini Kenya ambapo mradi huo mkubwa wa kilimo cha vanilla uko katika mji mdogo wa Mariakani kilomita 40 kutoka jiji la Mombasa.

Mradi huu unafanyika kwa ushirikiano na Mabati Technical Training Institute na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo Safaricom Foundation ya nchini Kenya.
 
“Safari ya kilimo cha Vanilla inaenda vizuri licha ya vikwazo vya hapa na pale vya kisiasa lakini kiukweli wakenya wamekipokea kilimo cha vanilla kwa jicho kubwa sana hususani wakenya wanaoishi katika nchi mbalimbali za ughaibuni”, amesema Simon Mnkondya Mkurugenzi wa kampuni ya Vanilla International Limited yenye mashamba yake pia Nchini Tanzania katika eneo la Zanzibar , Arusha na Dodoma.
 
Kwa Upande wa wakenya wamesema mradi huo utakuwa mkombozi wa uchumi wa Kenya na chanzo kikubwa cha ajira na kutoa ahadi ya kuwa watatunza vanilla vizuri na kushukuru kwa elimu ya utunzaji wa vanilla kutoka Mkurugenzi wa kampuni ya Vanilla International Limited Simon Mnkondya (+255 629 300 200).
Previous articleBARRICK YAWEZESHA DAWATI LA KIJINSIA NA WATOTO KUTOA ELIMU YA KUTAMBUA NA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI
Next articleWAZIRI MKUU AKIWA KIJIJINI KWAKE NANDAGALA RUANGWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here