Home BUSINESS MIAKA 3 YA Dkt. SAMIA, OFISI YA MSAJILI WA HAZINA YAKUZA MAPATO...

MIAKA 3 YA Dkt. SAMIA, OFISI YA MSAJILI WA HAZINA YAKUZA MAPATO YA TAASISI INAZOSIMAMIA

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Msemaji wa Serikali Mobhare Matinyi, amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, thamani ya uwekezaji katika taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina imeongezeka kutoka shilingi trilioni 70 mwaka 2021 hadi kufikia shilingi trilioni 76 mwaka 2023 – sawa na ongezeko la asilimia 8.6.

Matinyi ameyasema hayo alipokuwa akiizungumza na wahariri na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan madarani, katika mkutano uliofanyika leo Machi 24,2025 Jijini Dar es Salaam.

Ametaja sababu ya ongezeko hilo kuwa ni Serikali ya Awamu ya Sita kuongeza mitaji kwa kiasi cha shilingi trilioni 5.5 katika mashirika ya kimkakati kwa maslahi ya Taifa.

Aidha amesema kuwa Ofisi ya Msajili wa Hazina pia imeongeza makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi kutoka shilingi bilioni 637.66 hadi trilioni 1.008 kwa mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 58.

Akizungumzia umiliki wa hisa katika Kampuni zenye ubia, amesema Serikali imeongeza hisa zake ambapo katika Kampuni ya almasi ya Williamson Diamonds zimeongezeka kutoka asilimia 25 hadi 37, huku ikisaini mikataba ya ubia wa asilimia 16 zisizohamishika katika kampuni za madini,

Previous articleWAZIRI MKUU AKIWA KIJIJINI KWAKE NANDAGALA RUANGWA
Next articleDK. NCHIMBI: SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA NI MAISHA YA WATU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here