Home BUSINESS DKT. NCHIMBI ASHIRIKI MKUTANO WA 11 WA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA RAFIKI...

DKT. NCHIMBI ASHIRIKI MKUTANO WA 11 WA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA ( FLMS)


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akizungumza wakati wa kutoa salaam za CCM za mshikamano kwenye Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika (FLMS), leo Jumatatu, Machi 18, 2024. Mkutano huo unaofanyika katika Mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe, umewakutanisha Makatibu Wakuu wengine wa vyama hivyo rafiki, ambao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia) Komredi Sophia Shaningwa, Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Komredi Fikile Mbalula, Komredi Roque Silva Samuel (FRELIMO – Msumbiji), Komredi Paulo Pombolo (MPLA – Angola), Komredi Kavis Kario (BDP – Botswana) na Komredi Albert Mpofu (ZANU – PF – Zimbabwe), ambaye ni mwenyeji na mwenyekiti wa mkutano huo.Mkutano wa 11 wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika (FLMS), unaowakutanisha wajumbe wake, ambao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia), Komredi Sophia Shaningwa, Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Komredi Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO (Msumbiji), Komredi Roque Silva Samuel, Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA (Angola), Komredi Paulo Pombolo, Katibu Mkuu wa Chama cha BDP (Botswana), Komredi Kavis Kario na Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU – PF (Zimbabwe), Komredi Albert Mpofu, (mwenyeji na mwenyekiti wa mkutano), ukiendelea kujadili agenda, leo Jumatatu, Machi 18, 2024, katika ukumbi ulioko Mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe, unakofanyikia.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi (wa pili kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja, leo Jumatatu, Machi 18, 2024, pembezoni mwa siku ya kwanza ya Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, unaofanyika katika Mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe. Makatibu Wakuu wengine pichani, (kutoka kulia) ni Komredi Roque Silva Samuel (FRELIMO – Msumbiji), Komredi Paulo Pombolo (MPLA – Angola), Komredi Albert Mpofu (ZANU – PF – Zimbabwe, mwenye suti), Komredi Sophia Shaningwa (SWAPO – Namibia) na Komredi Fikile Mbalula (ANC – ANC).

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi (kushoto) kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia) Komredi Sophia Shaningwa (katikati) na Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Komredi Fikile Mbalula (kulia), wakionesha alama ya salaam za CCM, Chama cha ANC na Chama cha SWAPO, leo Jumatatu, Machi 18, 2024, pembezoni mwa siku ya kwanza ya Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, unaofanyika katika Mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe. Makatibu Wakuu  wa Vyama wengine wanaoshiriki mkutano huo ni pamoja na Komredi Roque Silva Samuel (FRELIMO – Msumbiji), Komredi Paulo Pombolo (MPLA – Angola), Komredi Kavis Kario (BDP – Botswana) na Komredi Albert Mpofu (ZANU – PF – Zimbabwe), ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo.
Previous articleWAZIRI MAVUNDE AZINDUA BARRICK ACADEMY KATIKA MGODI WA BUZWAGI ULIOFUNGWA
Next articleGETHSEMANE GROUP KINONDONI(GGK) WAACHIA VIDEO YA BWANA WASTAHILI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea DKT. NCHIMBI ASHIRIKI MKUTANO WA 11 WA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA ( FLMS)